Kipimo Abdallah
WANACHAMA
75 kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Msasani
Jimbo la Kawe akiwemo Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake Chadema
Kawe (BAWACHA) wamejiunga na chama cha Alliance for Change and
Transparent (ATC-Tanzania).
Hayo
yamebainishwa na Mwenyekiti wa ACT-Tanzania Mkoa wa Dar es Salaam
Khamis Chambuso wakati akiwakabidhi kadi za chama hicho leo jijini Dar
es Salaam.Chambuso
alisema wanachama hao pamoja na wanachama wengine kutoKA Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na CHAUMA wamejiunga na ACT- Tanzania kwa mapenzi yao
bila kushawishi na kitu chochote.
Alisema
kwa siku jana wamepokea wanachama 78 ambapo mmoja anatokea mkoa wa
Kigoma na wengine wanatokea mkoa wa Dar es Salaam wengi wao wakiwa ni
kutoka CHADEMA.
“Kimsingi
tunajisikia faraja kuona Watanzania waliowengi wanaanza kutambua
umuhimu wetu na wameamua kujiunga na ACT- Tanzania hivyo wanatuongeza
nguvu ya kufanya mabadiliko ya nchi”, alisema.
Alisema
ACT-Tanzania kina dhamira yua kweli ya kuhakikisha kuwa mfumo mzima wa
nchi unabadilika ikiwa nin pamoja na kushirikisha jamii ya Watanzania
inafaidika na rasilimali zilizopo hapa nchini.
Chambuso
alisema ACT- Tanzania haijaja kwa ajili ya kubomoa vyama vingine ila
misingi yake ndio chanzo cha watu kutoka vyama mbalimbali kuhitaji
kujiunga nao.
Mwenyekiti
huyo aliwataka wachama hao wapya kuhakikisha kuwa ni sehemu ya
mafanikio ya ACT-Tanzania kwa kuongeza wanachama zaidi.
Kwa
upande wake Mhandisi Mohammed Ngulangwa ambaye ni kada wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) wa siku nyingi tangu mwaka 1997 alisema kilichomuondoa
CCM ni chama hicho kushindwa kutekeza sera zake.
Ngulagwa
ambaye mwaka 2010 aliingia katika kinyang’anyiro cha kugombea Ubunge
ndani ya chama Jimbo la Temeke alisema kimsingi chama cha ACT-Tanzania
ndicho chenye misingi sahihi ya kidemokrasia.
Alisema
juhudi zake katika siasa atazionyesha kwa nguvu zote ili kuhakikisha
kuwa chama hicho kipya kinafanya vizuri katika medani za siasa hapa
nchini.
No comments:
Post a Comment