Jasmine Tridevil katika pozi.Jasmine
ambaye ni raia wa Tampa jijini Florida nchini Marekani
anayejishughulisha na utoaji huduma ya massage, alilipa kiasi cha dola
za Kimarekani 20,000 sawa na milioni 33.4 za Tanzania kufanyiwa upasuaji
huo.
Mwanamama huyo katika mahojiano na Real
Radio 104.1 alidai kuwa ameamua kufanya hivyo ili asiwe na mvuto kwa
wanaume maana hataki kuwa na mpenzi huku akipenda kuwa staa katika TV
japo
alipoulizwa sababu ya kwa nini hataki kuwa na mwenza hakutaja sababu.
alipoulizwa sababu ya kwa nini hataki kuwa na mwenza hakutaja sababu.
Takribani madaktari 50 walikataa
kumfanyia upasuaji huo wakiogopa kuvunja miiko ya fani yao hivyo
kumchukua miaka miwili kumpata daktari aliyekuwa tayari kufanya hivyo.
Kwa sasa mama huyo anarekodi video itakayoonesha changamoto anazokutana nazo akiwa mwanamke mwenye matiti matatu.
Mtaalam aliyemfanyia upasuaji ambaye
hakutaka kutajwa jina lake alichukua tishu katika tumbo la mama huyo ili
kutengeneza titi la tatu.
Jasmine amesambaza picha zake mpya akiwa katika vazi la bikini kupitia ukurasa wake wa Facebook baada ya upasuaji huo.
Mrembo huyo amedai kuwa amekanwa na mama yake mzazi pamoja na dada yake.
"Mama yangu alikimbia, hataki kuongea na mimi wala hataki dada yangu aongee na mimi baada ya kuongeza titi la tatu," Alisema Tridevil
"Mama yangu alikimbia, hataki kuongea na mimi wala hataki dada yangu aongee na mimi baada ya kuongeza titi la tatu," Alisema Tridevil
Mbali na furaha aliyonayo mrembo huyo,
bado anadai titi lake la tatu halifanani na mengine. Tridevil
analazimika pia kujitengenezea mavazi yake mwenyewe ambapo ananunua
mavazi mawili ya kuogelea
kisha moja analikata ili kupata nguo itakayokaa kwenye titi lake la tatu.
kisha moja analikata ili kupata nguo itakayokaa kwenye titi lake la tatu.
No comments:
Post a Comment