Tarime.
Watu 12 wamejeruhiwa wakati wa mashambulizi ya kurushiana risasi baina
ya askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) Kikosi 128 KJ cha Nyandoto na
Polisi wa Kituo cha Stendi wilayani Tarime mkoani Mara.
Mashambulizi hayo ya kurushiana risasi na kutwangana ngumi na mateke yalitokea juzi saa 12 jioni katika Kituo cha Polisi Stendi.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime, Bernard Makonyo
alisema amepokea majeruhi 10, kati ya hao wawili ni askari wa JWTZ,
polisi saba na raia mmoja. Alisema majeruhi tisa wameruhusiwa na
mwingine kupelekwa Hospitali ya Shirati kwa matibabu zaidi.
Dk
Makonyo aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni Aloyce Filbert (24) aliyepigwa
risasi mguu wa kulia, Deodatus Dominic (26) aliyejeruhiwa puani na wote
ni askari wa JWTZ.
Wengine
ni askari polisi saba ambao ni Makoye Katula (26), Sylvester Michael
(31), Salum Omary (44), Abdallah Halifa (24), Joel Msabila (25), Ally
Juma (27) na Deogratius Tryphon (32) na raia Hamza Jumanne (33)
aliyepigwa risasi mguu wa kushoto ambaye alipelekwa Hospitali ya
Shitari, Rorya kwa matibabu.
Mkuu
wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya, Ndalama Salumu anadaiwa
kujeruhiwa kwa kupigwa katika vurumai hizo huku mwananchi mwingine,
David Kisaro (20) akijeruhiwa kwa bomu jichoni. Alitibiwa katika
Zahanati ya Tarime.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya, Benedict Mambosasa alisema
mwanajeshi aliyekamatwa alifanya makosa kwani baada ya kukamatwa na
kuombwa kwenda kituo cha polisi, alikaidi.
Mambosasa
alisema mwanajeshi huyo licha ya kukiuka taratibu, aliwatolea lugha za
matusi polisi jambo lililowalazimu kumkamata kwa nguvu, ndipo wanajeshi
wenzake walipoingilia kati na kusababisha kutokea kwa majibishano ya
risasi za moto. Hata hivyo, alisema hakuna aliyejeruhiwa.
Alisema wanajeshi watatu ambao hawakutajwa majina, wamekamatwa na polisi kwa kuvunja utaratibu wa usalama.
Mkuu
wa Wilaya ya Tarime, John Henjewele ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, amelaani kitendo hicho cha kurushiana
risasi za moto hewani akisema ni cha utovu wa nidhamu na maadili ya kazi
ya jeshi na kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Alisema
wananchi Tarime wameshangazwa kwa kitendo kilichofanywa na walinda
usalama hao, wakisema si cha kinidhamu huku wakisema kilikwamisha
shughuli zao kwa muda kwa kuhofia usalama wa maisha yao.
Mkazi wa Tarime, Joseph Samson amesema kitendo hicho kimewashangaza sana wananchi.Chanzo Mwanachi Online
No comments:
Post a Comment