Mbongo Fleva, Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, na Vanessa Mdee wakila
'good time'. Tukio la kudhihirisha kwamba wawili hao ni wapendanao
lilitokea juzikati walipokuwa kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta katika
Mikoa ya Iringa na Morogoro ambako paparazi wetu aliwafuatilia hatua kwa
hatua.Chanzo chetu kilicho karibu na wawili hao kilipigilia msumari wa
uwepo wa penzi motomoto kati ya wawili hao kwa kudai hata ukaribu wa
msanii Jux na Vanessa ulioripotiwa hivi karibuni katika vyombo vya
habari, ulikuwa ni upambe tu kwa Dimpoz.
Mwanadafada wa Bongo Fleva Vanessa Mdee, akibadilishana mawazo na
Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’. “Jux alikuwa mpambe tu kwa Dimpoz wala hakuwa
na uhusiano na Vanessa kama wengi walivyokuwa wakifikiri,” kilisema
chanzo hicho.
Mara baada ya paparazi wetu kuwafotoa picha kibao zinazowaonesha
wawili hao wakipeana kampani ya karibu kwa nyakati tofauti katika ziara
hiyo, alimvaa Dimpoz na kumuuliza kama ndiyo ameamua kujisevia moja kwa
moja au vipi, msikie alichojibu:
Wakikonga vyoyo za mashabiki. “Ujue kuna vitu unaweza kujitahidi sana
kubishana na watu lakini kuna muda inabidi uwe mpole tu kama hii ishu
yangu na Vanessa maana walishaongea sana juu ya uhusiano wetu, sasa
nashindwa hata namna ya kumwepuka.
“Hatujawahi kugombana hata siku moja na sina jinsi ya kuepuka kufanya
naye chochote maana kama ishu ya mapenzi kati yetu ipo wazi na hakuna
jipya ambalo naweza kusema watu wakanielewa,” alisema Ommy
Dimpoz.Alipoulizwa Vanessa kuhusiana na uhusiano wao, aliishia kucheka
tu na kudai hakuwa na cha kuzungumza.
No comments:
Post a Comment