Mwanamuziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
KUFUATIA varangati lililotokea Tabora katika Tamasha la Serengeti
Fiesta 2014, baada mpenzi wa mwanamuziki wa mduara, Zuwena Mohamed
‘Shilole’, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kukataliwa na mashabiki, Shilole
ameamua kufunguka kuwa Nuh atabaki kuwa mpenzi wake katika hali yoyote.
Akizungumza na paparazi wetu, Shilole alisema lengo lake lilikuwa ni
kumtambulisha mpenzi wake kwa mashabiki wake japo walimkataa kuwa
shemeji yao.
‘Shilole’ akiwa na mpenzi wake 'Nuh Mziwanda'. “Wakati namtambulisha
Nuh kwa wakazi wa Tabora kuwa shemeji yao kiukweli nilishindwa kuelewa
kwa nini nilizomewa ila ninachoweza kusema tena wakubali, wakatae Nuh
atabaki kuwa shemeji yao tu,” alisema Shilole.
No comments:
Post a Comment