Mkali wa Bongo Flava Tanzania Diamond
Platnumz amepewa nafasi ya kushirikiana na Mziiki kama Brand Partner.
Msanii huyu ambaye amefanikiwa kushinda tuzo mbalimbali amekuwa wa
kwanza kutia saini kama Brand Partner na tayari ni mmoja wa mamia ya
wasanii pekee wa Afrika walio katika program ya muziki unaopendwa zaidi
Afrika kupitia simu za kiganjani pamoja na kuwa mwakilishi wa bidhaa
hiyo akiwakilisha nchi yake.
“Tunafurahi kwamba Diamond Platnumz kwa sasa ni Brand Partner wa
Mziiki,” anasema Arun Nagar, Mkurugenzi Mtendaji wa Spice VAS Africa,
watengenezaji wa Mziiki. “Kwa kushirikiana na msanii mwenye kiwango
kama Diamond pamoja na mashabiki wake ni hatua nzuri kwa Mziiki.
Ushirikiano kama huu unaonyesha dhamira yetu ili kuendelea kuhakikisha
kwamba watumiaji wetu na muziki bora wa Afrika unawafikia pale walipo
na tutaweza kufanya kazi karibu na Diamond na kupanua wigo wa wateja
wetu na kuwapatia mashabiki wake zaidi ya kile walichotarajia. Nadhani
pia ni ushahidi wa ukweli kwamba sisi tumechukua nafasi kubwa katika
ulimwengu wa muziki streaming na wapenzi wa muziki wa Afrika wanapaswa
kukumbuka hilo. ”Partnership between Bongo flava super star and music streaming app
Mziiki. Diamond shakes hands with Arun Nagar CEO for Spice VAS Africa
creators of Mziiki.
Pichani ni Babu Tale Diamond Meneja, Arun Nagar CEO & Michael Mlingwa
Mziiki ni huduma pekee inayokupa Miziki ya kiafrika kupitia Streaming,
huduma ambayo inatoa safu mbalimbali ya muziki kutoka Afrika na
kimataifa. “Mimi nimepata mzuka kujiunga na Mziiki,” anasema Diamond.
“Programu na simu (mobi) tovuti ni nafasi kubwa kwa ajili ya wasanii
kupanua idadi yao ya mashabiki na kutambulisha mara ya kwanza single
yao mpya kusikika bara la Afrika na dunia.”
Mziiki ni programu ya simu iliyoundwa kwa ajili ya Music Streaming
iliyosheheni miziki ya Afrika. Imepata umaarufu haraka ikiwa na
mkusanyiko mkubwa wa sauti safi na vipaji kipekee vinavyokidhi miziki ya
kiafrika.Programu hii ni rahisi kutumia,ina makala ambayo huruhusu
mtumiaji kushirikisha marafiki wimbo waupendao au kuwatumia nyimbo
kama miito ya simu ya nyimbo walizochagua. Makala haya yamewekwa
kuwawezesha wasanii, kama Diamond, kufikia mashabiki wapya katika
Afrika na duniani kote.
“Mziiki kweli imenipa zaidi ya kile ambacho ningeweza kuomba” Anasema
Diamond. “Mimi si tu kuwapatia mashabiki wangu nafasi ya kupata nyimbo
zangu zote bali pia pia kupata nafasi ya kupanua wigo wa mashabiki
wangu kupitia programu ya “Share and Dedicate” . Wakati mashabiki wangu
wakishirikisha au wakituma wimbo wangu wowote maalum kwa wenzao,nani
ajuaye waweza kusambaa kwa kiasi gani? Mimi tayari nimeshaanza kuona
idadi ya mashabiki wangu ikiongezeka kwa namna hii.
Ikiwa na kiwango kizuri na kuongezeka kwa orodha ya wasanii
waliosajiliwa kutoka katika bara la Afrika, Mziiki ni mahali ambapo
wasanii wapya wanaweza kwenda kuzindua kazi zao na wasanii waliopo sasa
kuendelea kukua.
Mziiki ni program ya Mobile Streaming iliyoundwa ili kukidhi
mahitaji ya msanii na mashabiki kwa jumla. Mziiki ilianzishwa mwezi Mei
2014, na imesaidia kuongeza mafanikio katika kazi za wasanii na
inaendelea kukua kila siku na kuwawezesha wasanii kufurahia zaidi kama
ilivyo kwa Diamond Platnumz..
No comments:
Post a Comment