YALE madai kuwa sexy lady wa Bongo Fleva aliyeibukia kwenye Shindano
la Kutafuta Vipaji la Epiq Bongo Star Search 2012, Meninah Abdulkareem
ya kutaka kuolewa na staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’ yamemtoa machozi mwanadada huyo.Sexy lady wa Bongo
Fleva aliyeibukia kwenye Shindano la Kutafuta Vipaji la Epiq Bongo Star
Search 2012, Meninah Abdulkareem. Hivi karibuni Meninah na Diamond
walizua na bado wanaendelea kuzua mjadala kila kukicha ambapo taarifa
juu ya wawili hao kutaka kufunga ndoa ya chinichini zinaendelea kusambaa
kwa fujo ambapo mwanadada huyo amelonga na Amani kwa dakika kumi.
Kikizungumza kwa kujiamini, chanzo makini ambacho kiliomba hifadhi ya
jina kilidai kwamba hakuna ndoa tena kati ya Diamond na Beautiful
Onyinye, Wema Isaac Sepetu na kwamba ndoa inayopangwa kwa sasa ni ya
Meninah na Diamond.
Chanzo hicho kilinyetisha kwamba wawili hao walikutana kwa mara ya
kwanza kwenye sherehe za utoaji wa Tuzo za Kili mwaka 2014 na tangu hapo
wamekuwa na ukaribu unaodaiwa unataka kuzaa ndoa.
WEMA AMWINDA
Ilisemekana kwamba baada ya Wema kuzinyaka habari hizo kuwa anataka
kunyakuliwa ‘beibi’ wake mbaya zaidi wanataka kufunga ndoa, malkia huyo
mkubwa wa sinema Bongo aligeuka mbogo na kuanza kuweka mikakati ya
kumteketeza Meninah asiweze kufunga ndoa na Diamond.
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Kuna
madai kwamba Meninah aliposikia Wema anamsaka usiku na mchana ili
amshikishe adabu, msanii huyo alishtuka kwa kuwa anaujua vizuri ‘mziki’
wa staa huyo.
VIKAO VYA HARUSI VYAFANYWA
Taarifa ziliendelea kudai kwamba, vikao vya harusi vya chinichini
vinaendelea kufanywa huku wahudhuriaji wakiwa ni mdogo wa Diamond ambaye
pia ni mwanamuziki, Mwanahawa Abdul Juma ‘Queen Darlin’ pamoja na
baadhi ya ndugu wa upande wa mama Diamond ambao wamekuwa wakifanya kila
wawezalo kuhakikisha ndoa hiyo inafungwa.
POMBE NA STAREHE VYATAJWA
Sababu kubwa inayosemekana Wema kutemwa kuolewa na Diamond ni
kutokana na kuendekeza pombe na starehe jambo ambalo Meninah yupo nalo
kando na kwamba hivi sasa amekuwa akitimba kwa mama Diamond bila
wasiwasi huku akizama jikoni kupika, kupakua na kufanya kazi ndogondogo
za ndani ili kuthibitisha kuwa yeye ni mama bora.
DIAMOND AMTOA MACHOZI
Baada ya kunyaka madai hayo, Amani lilimsaka Meninah na kumhoji juu
ya sakata hilo la kutaka kuolewa na Diamond ambapo alikuwa na haya ya
kusema:
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu. “Yaani sijui hata nianzie wapi
kuzungumzia hili la kutaka kufunga ndoa na Diamond, naomba niseme ukweli
kwamba nashangaa, kwanza sijui chochote, nimekuwa nikiandikwa mara kwa
mara lakini taarifa hizo wala hazina ukweli wowote.
“Mimi na Diamond ni tofauti kabisa, sijawahi kuwa na ukaribu naye.
Kwanza naumia sana na kutokwa na machozi kuendelea kusikia taarifa hizi
kuwa naolewa naye kitu ambacho hakipo kabisa, hata yeye mwenyewe
akisikia hivi anaweza kumtafuta mtu ambaye anasemwa kuwa anatoka naye
jambo ambalo si la kweli.”
“Wema namheshimu kama dada yangu, mtu ninayemjua kwenye tasnia ya
filamu Bongo, kwanza wote tunafanya sanaa japokuwa kwa upande wake
anafanya filamu na mimi muziki. Hizo taarifa juu ya kuniwinda sijui na
sijazisikia. Kiukweli zimenishtua sana.”
Diamond alipotafutwa kuzungumzia ishu hiyo hakupatikana kwa kuwa alikuwa ziarani barani Ulaya.TUJIKUMBUSHE
Kwa wiki kadhaa sasa, Meninah na Diamond wamekuwa wakihusishwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi.
No comments:
Post a Comment