SAKATA la mtoto Happiness (10) aliyetikisa kwa tukio la kupanda ndege
kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Zanzibar bila kujulikana limeibuka
tena, safari hii katika sura mpya kufuatia mtoto huyo kufungua kinywa
chake na kuanika mambo ya kichawi, Uwazi lina mkanda mzima.Mtoto
Happiness (10) anayeishangaza jamii kwa matukio ya kimazingara. Mtoto
huyo aliyaanika mambo hayo mwishoni mwa wiki iliyopita mbele ya Kamanda
wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Dar, SACP Mary Nzuki na kumfanya afande huyo
kupigwa butwaa. Aidha, alizungumza na Uwazi, nyumbani kwao, Mkuranga.
ALICHOSEMA AWALI NI HIKI
Awali akizungumza kwa kujiamini, mtoto huyo ambaye ni mkazi wa Kijiji
cha Mkokozi Kata ya Vikindu wilayani Mkuranga, Pwani, alikiri kusafiri
kwa ndege hadi Zanzibar akidai alikwenda kumfuata baba yake mzazi
aishiye huko.
Hata hivyo, mama yake mzazi, Sarah Zefania alimpinga mwanaye huyo na
kusema: “Baba yake haishi Zanzibar, yupo Kipunguni (Ilala jijini Dar es
Salaam).”
Mtoto Happiness akiwa na mama yake KUHUSU UCHAWI
Mtoto Happiness alikwenda mbele zaidi kwa kujiongeza akisema katika
maisha yake amekuwa akifanya mambo ya kishirikina lakini si peke yake.
Alisema ana mshirika wake (hakumtaja jina)
Happiness aliutaja ushirikina huo. Alisema amekuwa akisafiri usiku
mara kwa mara na mshirika wake huyo wa karibu kwa kutumia usafiri wa
ungo!!
ATAJA PAKA, NYOKA NA MBUZI
Kama vile haitoshi, mtoto huyo ambaye ametokea kushangaza wengi
hukuakipachikwa majina ya ‘mtoto wa ndege’, ‘mtoto wa uchawi’ na ‘mtoto
wa miujiza’, alisema akiwa katika safari hizo amekuwa akiwaona paka,
nyoka na mbuzi.
AFIKA POPOTE BILA KUJALI UMBALI
Aliongeza kuwa, kwa kutumia ungo na huyo mshirika wake, wamekuwa na uwezo wa kufika popote wanapopataka bila kujali umbali.
Mkoba ukiwa na nguo za Mtoto Happiness MAVAZI YA SAFARINI
Akizidi kufunguka, Happiness alisema mara nyingi wanapokuwa katika
safari hizo ambazo alisema watu hawawezi kuwaona, huvaaa nguo nyeupe,
nyeusi au wakati mwingine nguo nyekundu ili kufanikisha masuala yake ya
usiri.
Mtoto huyo aliyasema hayo kufuatia Septemba 16, mwaka huu kudakwa
tena maeneo ya Feri jijini Dar akiwa na begi ambapo alisema anamfuata
baba yake (hakusema wapi).
Baada ya walinzi wa eneo hilo kumgundua ni ‘mtoto wa ndege’
walimfikisha Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar ambapo mama yake
aliitwa.
Mama alishtuka baada ya kumwona mwanaye akiwa amebeba begi lililokuwa
na nguo kwa madai ya kuwa alikuwa akielekea kwa baba yake mzazi.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Dar, SACP Mary Nzuki SIKU YA KUTOROKA MARA YA PILI
Akisimulia kisa cha kutoroka mara hii ya pili, Happines alisema siku
ya tukio mtu mmoja ambaye alidai kuwa ni kaka yake wa kambo alifika
nyumbani na kumchukuwa yeye na begi lake la nguo akidai anampeleka kwa
baba yake Zanzibar lakini baada ya kufika Feri mtu huyo alitokomea
kusikojulikana. KAULI YA MAMA
Wakati mama huyo (pichani) akizungumza na Uwazi alimtaka baba wa
mtoto huyo, Julius kujitokeza ili kunusuru hatima mbaya ya mtoto wao.
WACHUNGAJI WANENA
Waandishi wetu waliwatafuta baadhi ya wachungaji wa makanisa ya kiroho nchini ili wazungumzie tukio la mtoto huyo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zakary Kakobe. NI MAPEPO
Mchungaji wa Kanisa la Paradise International la jijini Dar, Gideon
Parapanda alisema tatizo linalomsumbua mtoto huyo ni pepo mchafu wa
kuzimu hivyo kwa kutumia maombi ndani ya makanisa hali hiyo itatoweka.
“Happiness kama alizaliwa salama na hali hiyo imemkuta ukubwani na
kufanya mambo ambayo hayaeleweki ni pepo wachafu ambapo akimtumainia
Yesu tatizo hilo litaisha mara moja,” alisema Mchungaji Parapanda.
WAZAZI WASIENDE KWA WAGANGA
Naye Mchungaji wa Kanisa la Cathedral of Joy, pia ni Nabii John
Komanya, yeye alisema Happiness anasumbuliwa na pepo wachafu, kitu pekee
ni maombi na alitahadharisha wazazi au ndugu wasiende kwa waganga wa
kienyeji.
ASKOFU KAKOBE ATAKA APELEKWE FULL GOSPEL
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zakary Kakobe
yeye alisema matatizo ya Happiness yataisha kwa Jina la Yesu kama ndugu,
walezi au wazazi wataamua kumfikisha kanisani kwake.
“Kinachomsumbua mtoto huyo ni roho chafu, akiombewa katika makanisa
ya kiroho atafunguliwa, hata kama ndugu wakiamua kumleta hapa Full
Gospel ni sawa tu, atakombolewa,” alisema Kakobe.
No comments:
Post a Comment