Taarifa
zimethibitishwa kuhusu staa wa hit single kama ‘pombe yangu’ ‘tema mate
tuwachape’ na ‘ni shidaah’ Madee ambae ni msanii kutoka kundi la TipTop
Connection kushikiliwa na Polisi.
Kabla ya kuongea na meneja wa kundi hilo ambae ni Babtale, Gossip Cop
Soudy Brown kwenye You heard inayosikika kupitia XXL ya CloudsFM
J3-Ijumaa alisema ‘inasemekana Jumamosi iliyopita Madee aliporwa simu
yake na watu wawili usiku huko Kigamboni’Babtale alipoulizwa akasema
‘Kwenye mida ya saa tisa usiku Madee wakati anatoka kwenye show
Kigamboni kuna waporaji simu wakiwa kwenye pikipiki wakampora kwa hiyo
ikabidi gari aliyokuwemo Madee ikiendeshwa na Kwebe ianze kuikimbiza ile
pikipiki alafu wakaigonga pikipiki kwa nyuma, pikipiki ilivyodondoka
yule aliekua nyuma kwenye pikipiki ambae ndio alipora simu akafanikiwa
kukimbia hivyo wakaishia tu kumkamata aliekua anaendesha hiyo pikipiki’
‘Wakamchukua na kwenda nae maskani Tiptop… mama yake akaja akasema
msipeleke Polisi mwekeni hapa mi nakwenda kuwachukulia vitu vyenu, Madee
kwa sababu alikua anakwenda kwenye show Mwanza ikabidi aende zake…… saa
nne asubuhi yule mama akaja na Polisi badala ya kuja na mwizi mwenzake
akaja na Polisi kataka kuwaokota watoto wote ofisini kwangu pale Tiptop,
walimchukua huyo Muhalifu kwenye Land rover mpaka Polisi Magomeni na
kubadilisha kibao kwamba huyu mtuhumiwa alitekwa’
‘Alipigwa akaumia hivyo wakamuombea PF3 wakampeleka Hospitali,
nikapigiwa simu na Madee kwamba anatakiwa Polisi akaripoti…. kufika
kituoni wakakuta ile pikipiki na kukuta yule dogo ndio anafika kutoka
Hospitali akawaambia huyu ni mwizi ameiba, ikabidi Dogo aingizwe ndani
jana akalala pale Polisi Magomeni’
‘Asubuhi yake Madee akaenda kituoni kama kufata Mwalifu wake na
kutaka simu yake aliyoibiwa, akaambiwa kesi inabidi ihamishiwe
Kigamboni…. saa kumi na mbili jioni ndio Kwebe ananitumia msg anasema
Madee analalamika mbona humfatilia nikauliza kuna nini tena akasema
wamemuingiza ndani, nikapiga simu Polisi Kigamboni ndio wakaniambia
kijana wako tulitaka kumtoa lakini hatuwezi sababu amemteka mtu,
nikapiga simu kwenye vyanzo vyangu vya msaada tukamtolea dhamana…. ni
hilo, yataisha kama yalivyoanza’
No comments:
Post a Comment