Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.
Mitandao
ya kijamii ni mizuri katika kuhabarisha umma endapo inatumiwa kulingana
na madhumuni iliyotengenezwa, kwani ina nguvu ya kusambaza habari kwa
haraka na kwa wakati hapa duniani.
Pamoja
na umuhimu nwa mitandao hii ya kijamii, kuna baadhi ya watu ambao wao
hujiona kuwa wameendelea katika ulimwengu wa kisayansi na teknolojia
kiasi cha kuanza kuitumia mitandao hiyo kinyume na malengo kwa kutumia
kuiba taarifa mbalimbali za watu na hata usalama wa maeneo muhimu
ikiwemo benki, ofisini, mashuleni na sehemu kadha wa kadha.
Watu
hawa kwa jina la kisayansi na teknolojia hujulikana kama ‘Hackers’ au
Wezi wa mitandao kwa kisawahili, na wamekuwa wakivumbua mbinu mbalimbali
kila kukicha ili kuweza kutimiza adhma yao ya kuingilia mitandao mingi
iliyopo duniani na wakati mwimngine wamekuwa wakitumika katika shughuli
za kigaidi ulimwenguni.
Kwa
mujibu wa taarifa mbalimbali toka mitandaoni, kuna mbinu nyingi
zitumiwazo na hackers hawa katika kuiba taarifa mbalimbali kutoka kwenye
takirishi (Computer) hata simu za mkononi kwa njia ya mtandao
(internet) na njia hizi huwa zimekuwa zikiboreshwa kila kukicha.
Wezi
wa mitandao wengi wamekuwa wakitumia visaidizi vya kompyuta (softwares)
zijulikanazo kama Keyloggers ambazo ni hatari sana katika kuiba taarifa
toka sehemu yoyote endapo tu mmiliki wa kompyuta ataiacha kompyuta yake
kutumiwa na watu wasiofahamika ama katika ofisi mtu mharibifu ataingia
na kuingiza katika mfumo wa kuongozea kompyuta kisaidizi kama hiko,
kutokana na hilo software hizo hukusanya taarifa za mtu pasipo mtumiaji
kujua kinachoendelea na taarifa hizo hutumwa kwa njia ya barua pepe
kwenda kwa mharifu ambaye yeye anakuwa anazipata kadri atakavyo juu ya
chochote akifanyacho mtu, na moja ya sifa za software hizo ni kwamba
hazionekani ndani ya mfumo wa kuongozea kompyuta kirahisi.
Mbinu
nyingine watumiazo watu hao ni kwa njia ijulikanayo kwa kimombo kama
‘Phising’ ambapo ukurasa unaofanana sawia na ukurasa halisi wa website
hutengenezwa kwa madhumuni thabiti ya kuiba nenosiri ama taarifa zozote
kuhusiana na kitu chochote, njia hii ni hatari pia ingawa haina tofauti
sana na njia ile ya key logging kwani katika njia hii kazi kubwa
inayofanyika ni kuweko kwa kurasa feki ambayo inayofanana na kurasa
halisi ya website fulani.
Ili
tuweze kujikinga na matukio haya ya wizi wa taarifa kwa njia ya mtandao
kuna mambo muhimu ya kuzingatia ambayo tunapaswa kuwanayo makini wakati
wote tunapozitumia kompyuta zetu.
Kwaza
kabiasa, ili tuweze kujiepusha na njia itumiwayo na hackers ijulikanayo
kama Key-logging ni vema kuepuka kuazimisha kompyuta zetu kwa watu
tusiowajua ama kutumia mbinu ya kubofya kitufe cha Ctrl + shift + Alt + K
vyote kwa pamoja ili kuweza kujua uwepo wa kisaidizi kama hiko katika
kompyuta na kama ikitokea kimekuja kisanduku kinachokudai kuweka
nenosiri basi ujue hapo kuna mtu anachunguza taarifa zako katika
kompyuta yako pasipo wewe kujua, hivyo chukua tahadhari kwa kumtafuta
mtaalam aweze kuondoa kisaidizi hiko.
Pia yatupasa kuhakikisha kuwa Windows Firewalls zilizopo ndani ya mifumo ya kuongozea kompyuta zetu ziko wazi wakati wote kwani firewall inasaidia
kulinda takirishi yako dhidi ya wezi wa mitandao (hackers) ambao
wanaweza kujaribu kuiharibu kwa lengo la kutaka kupata taarifa zilizomo
ndani, kufuta taarifa, na hata kuiba baadhi ya neno siri za baadhi ya
taarifa zako.
Ili
kujikinga na wizi wa taarifa zetu katika kompoyuta zetu, tunapaswa
kuzingataia kuingiza ama ku-update Vizuizi virusi (Antivirus) mara kwa
mara kwani vizuizi hivyo vimetengenezwa
kwa ajili ya kuzuia virusi ama visaidizi kompyuta chokozi ili zisiweze
kuiingia ndani ya mfumo wa kompyuta na endapo ikitokea imegundua kirusi
cha namna yoyote ile, basi inafanya kazi ya kukiondoa ama kukifanya
kisiweze kudhuru kompyuta wakati wote.
Bila
shaka lolote, Virusi vinaweza kuharibu mfumo wa kuongozea kompyuta
pasipo mtumiaji mwenyewe kujua licha ya baadhi ya vizuizi virusi kuwa na
tabia ya kuji-update vyenyewe.
Kuweka ama ku-update Antispyware Technology ni jambo linghne la usalam dhidi ya hackers kwani Baadhi
ya spyware huwa na tabia ya kukusanya taarifa za mtu pasipo ridhaa yake
kama ilivyo kwenye key-logging na Phising au huwa na tabia yakuweka
matangazo yasiyo na ulazima katika kurasa Fulani iliyopo katika mtandao
wa kompyuta, sasa hii ni hatari kwa usalama wa taarifa za mtu kwani
hutumika pia kukwapua, hivyo hatunabudi kuwa makini na baadhi ya
matangazo yenye kututaka kupakua visaidizi fulani pasipo malipo kwani
mara nyingi huwa ni feki na wakati mwingine huwa na virusi vyenye kuweza
kutumika kuiba taarifa ndani ya takirishi yako.
Katika
hali yoyote ile ni vema kwa watumaiji wa mitandao ya kijamii kuepuka
kutunza nenosiri katika kompyuta zao kwa lengo la kuondoa usumbufu
wakati wanapotaka kuingia tena katika kurasa zao kwani njia hiyo nayo ni
hatari kwasababu mtu anapoacha nenosiri lake liko (logged in) au
unaposema (remember me next time) unatengeneza njia rahisi kwa hacker
kujua nenosiri lako kwa kufanya kitendo kijulikanacho kama (Inspect
elements Q) yaani zile doti zinazowakilisha neno siri lako (******).
Katiko
hilo, mharifu anachokifanya hapo ni kuhailaiti hizo doti (nyota) kisha
anabofya katika kipanya upande wa kulia (right clicking) kisha anaenda
mwisho katika sehemu iloandikwa (inspect elements Q) kisha
anafanya uhariri (editing) katika kipengele kilichokuwa hailaitedi kwa
rangi ya bluu kilichoandikwa neno ‘passoword’, hapo anafuta na kuandika
neno ‘TEXT’ kisha anabofya kitufe cha ‘Enter’ na akishamaliza kufanya
hivyo nenosiri lenyewe linajibadilisha kwenda mfumo wa maneno badala ya
doti kama ilivyokuwa hapo mwanzo, hivyo humuwezesha kujua tarakimu za
nenosiri la akaunti yako ya mtandao wa kijamii uliocha wazi.
Njia
nyingine ya jinsi ya kujikinga na wizi wa kimtandao, tunahitaji kuwa
makini na vitu tunavyopakuwa toka mitandaoni hasa vibebaji (attachments)
toka kwa watu tusiowafahamu au wakati mwingine kwa watu tunaowajua
kwani hata hao hutumika katika kusaidia kuibwa kwa taarifa zetu kwa
malengo yao binafsi.
Pia
ni vema kuepuka kukubali marafiki tusiowajua katika mitandao mingi ya
kijamii ikiwemo facebook, twitter, Whatsapp, na mingineyo kwani baadhi
ya hackers wanatumia majina yasiyosahihi (fake names) kuomba urafiki
kisha hutumia mwanya huo pia katika kuiba taarifa zetu kiurahisi.
Kwa
upande wa mabenki, ni vema kuachana na mifumo ya kizamani ya kuongozea
kompyuta iliyounganishwa na Mashine za kutolea fedha maarufu kama (ATM)
au Automatic Teller Machine kwa kimombo, kwani hiyo ni hatarishi
kwasababu mifumo ya kizamani, mfano Microsoft Windows XP ni mifumo
ilikwishapitwa na wakati na hata Kampuni yenyewe ya Microsoft imewataka
watumiaji kuwa makini nayo kwani haina-updates tena hali inayopelekea
kuwa katika hatari ya kuvamiwa na wezi wa mitandao kwa kutumia software
za kisasa zenye uwezo wa hali ya juu katika kuiba taarifa.
Katika
matumizi ya kadi zetu za kutolea fedha benki (ATM Cards) tunapaswa kuwa
makini kuepuka kushea namba za siri kwa marafiki au wapenzi na
tujitahidi kuacha tabia ya kutumia nenosiri la kadi hizo kama nenosiri
katika akaunti za mitandao ya kijamii kwani hackers nao wamekuwa watu
wazuri wa kubashiri taarifa pindi wanapomlenga mtu.
Ili
kujiweka salama dhidi ya wezi wa mitandao, basi tujitahidi kutoa
taarifa zozote za kiusalama kwa vyombo vya usalama yaani Polisi au
kupeleka malalamiko kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) pindi
tunapoona taarifa za uvunjwaji wa sheria za matumizi ya mitandao, mfano
mtu akiona kuna hitilafu katika taarifa za muamala wa fedha zake katika
akaunti yake ya benki fulani basi atoe taarifa kwa benki husika ili wao
waweze kutafuta tatizo na kutoa ufumbuzi.
Pamoja
na haya yote Watanzania wamehimizwa kuacha matumizi mabaya ya mitandao
ya jamii ikiwemo kuweka picha za utupu, kusababisha ugomvi, kuwahimiza
wengine kwa mambo yasiyo ya kweli, kupotosha jamii na kuvuruga
maendeleo.
Akitoa
rai hiyo Meneja mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),
Bwana Innocent Mungy alisema kuwa kuna ongezeko la matumizi ya intanenti
kwa watanzania hasa mitandao ya kijamii ambayo ni facebook, twiter,
Instagram, BBM, LinkedIn na Blogs mbalimbali kwa mambo yasiyofaa na
kuleta athari kwa jamii.
Alisema
matukio yanayofanyika katika mitandao hiyo na kuleta athari ni utapeli,
kulipiza kisasi na ugomvi unaoanzia mitandaoni na kuendelea hadi kwenye
uhalisia.
“Kuna
utapeli wa kutumia huduma za mawasiliano na ugomvi wa makundi
yakugombana kupitia mitandao kwa majina kama timu fulani na timu fulani
inayosababisha kuvunjika kwa amani na kusababisha matusi pande zote,”
alisema Mungy.
Mungy
aliongeza kuwa ni kosa la jinai kutumia mawasiliano vibaya kama
ilivyoainishwa katika sheria ya mawasiliano ya Kielektroniki na Posta
(EPOCA) ya mwaka 2010 na kutaka mawasiliano yatumike vizuri kudumisha
amani ya Tanzania.
“Mamlaka
inapenda kuukumbusha umma kuwa ni kosa la jinai kuuza laini ya simu
iwapo siyo wakala au mtoa huduma, kutumia simu isiyosajiliwa, kutumia
njia yeyote ya mawasiliano kuvuruga amani na kumsaidia mtu mwingine
atende kosa,” alisema.
Kwa
mujibu wa Mungy ni kosa la jinai kuweka picha za marehemu, mtoto na
zinazoonesha utupu katika mitandao ya kijamii huku akibainisha kwamba
faini ya kosa hilo ni shilingi za Kitanzania 750,000 na kifungo cha
miezi mitatu gerezani.
Kutokana na haya, lazima tutambue kuwa mitandao ya kijamii si dhambi wala si vibaya kuitumia, kwani haijatengenezwa kwa madhumuni ya kumkomoa fulani ama kwa lengo la kuelimisha watu juu ya namna ya kuiba taarifa za watu wengine, bali inetengenezwa ka madhumuni ya kuwakutanisha watu wa sehemu mbalimbali duniani kuweza kuhabarishana juu ya mambo mbalimbali japokuwa baadhi ya watu hao wamekuwa wakiitumia vibaya kinyume na maelngo ya uwepo wake
No comments:
Post a Comment