Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, msala huo ulijiri juzikati nyumbani
kwa ticha huyo, Kichangani ambapo mwalimu huyo alidaiwa kufumwa na mume
wa mtu, Raphael Bernard (33) ambaye ni dereva wa bodaboda.
KATIKA
hali ya kutisha, fumanizi lililoambatana na bonge moja la mtiti
linadaiwa kujiri nyumbani kwa mwalimu ‘ticha’ wa Shule ya Msingi ya
Mafisa ‘A’, iliyopo Manispaa ya Morogoro mjini hapa aliyefahamika kwa
jina la Rosemary Mkoba kisha watu wakachomana visu.
Habari
zilidai kwamba mwenye mume amekuwa akimfuatilia mumewe kwa muda mrefu,
akagundua huwa anakwenda kujichimbia kwa ticha huyo huku akiacha familia
ikilala njaa.
Ilisemekana
kuwa, siku ya tukio, mwenye mume, akiwa na ‘jeshi’ lake, alimfuatilia
mumewe hadi akamuona akiingia nyumbani kwa hawara wake huyo.
Ikazidi
kudaiwa kwamba baada ya kuhakikisha jamaa amelala kwa ticha huyo,
mwanamke huyo na ‘skwadi’ yake waliondoka, asubuhi iliyofuata mishale ya
saa 1:04 wakatia timu na kulianzisha timbwili huku mke huyo akidaiwa
kumtishia ticha kuwa akipata ujauzito atazaa kwa mdomo.Bw.
Raphael Bernard akiuguza majeraha hospitalini. Habari zinadai kuwa,
baada ya mke huyo na timu yake kuondoka, ticha huyo alimuwakia Raphael
kwamba kumbe ana mke, kwa nini hakuwahi kumwambia? Ugomvi mwingine
ukazuka hapo. PICHA ZAIDI>>
No comments:
Post a Comment