Nyota
wa sinema Bongo, Aunty Ezekiel akiwa Bongo. Kwa mujibu wa chanzo,
mwishoni mwa Februari, mwaka huu, Aunty alikwenda kwa Shabani na kuazima
cheni hiyo kwa makubaliano ya kuirejesha baada ya muda jambo ambalo
hakulifanya na baadaye, Septemba mwaka huu, akasafiri kwenda Marekani
kutangaza utalii wa ndani.
Baada
ya kurejea, Oktoba mwaka huu, Shabani alimkomalia Aunty na kufikishana
Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar ambapo staa huyo alisema na yeye
alimwazima cheni hiyo rafiki yake aitwaye Neema.
Ilidaiwa
kuwa, Neema baada ya kubanwa alikiri na kusema aliiweka bondi cheni
hiyo na hapo ndipo danadana zilipoanza hivyo jamaa akaamua kwenda
kufungua madai mengine Kituo cha Polisi Pangani.
Juatano
iliyopita, mapaparazi wetu walifunga safari mpaka kituoni hapo ambapo
baadhi ya askari walikiri kuwepo kwa kesi hiyo lakini waligoma kutoa
namba za kumbukumbu za jalada ‘RB’ wakidai mwenye uwezo huo ni Kamanda
wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova. SOMA ZAIDI>>>
No comments:
Post a Comment