
Wanajeshi wa Marekani wakiwa Kazini
Rais
wa Marekani Barrack Obama ametangaza mpango wake wa kuwatuma wanajeshi
3,000 Afrika Magharibi kama njia mojawap ya kusaidia katika vita dhidi
ya ugonjwa hatari wa Ebola.
Rais
Obama ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za dharura
kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Ebola Magharibi mwa Afrika ambao unaenea
kwa kasi sana.
Bwana
Obama amesema kuwa iwapo mlipuko wa maradhi hayo haukomeshwi kwa sasa,
mamia ya maelfu ya watu wataambukizwa na yatakuwa tishio kwa usalama wa
dunia.
Jemedari
mmoja wa Marekani amewasili nchini Liberia kuongoza wanajeshi hao 3,000
wa jeshi la Marekani waliotumwa eneo hilo kupambana na maradhi hayo.
Wanajeshi
hao watasimamia ujenzi wa vituo vipya vya kimatibabu na pia watahusika
katika utoaji wa mafunzo ya kimatibabu kwa wahudumu.
Kumekuwa
na malalamishi kwamba jamii ya kimataifa imelegea katika harakati za
kukabiliana na mkurupuko wa Ebole katika mataifa ya Afrika magharibi.
Mataifa
ya Sierra Leone, Liberia na Guinea ndiyo yaliyoathirika zaidi huku
zaidi ya watu 2,400 wakiwa tayari wamepoteza maisha yao kufikia sasa.
Zaidi ya nusu ya idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huu ni raia wa Liberia.
Shirika la afya duniani (WHO) limetahadharisha kuwa huenda watu zaidi wakazidi kufariki.
Umoja
wa Mataifa (UN) unapangiwa kuzungumzia jinsi ya kukabiliana na mlipuko
wa ugonjwa wa Ebola katika mkutano unaopangiwa kufanyika huko
Geneva.Chanzo BBC Swahili
No comments:
Post a Comment