Msichana wa miaka 18, raia wa India
aliyetajwa kwa jina la Mangli Munda amefunga ndoa na mbwa baada ya
kulazimishwa na wazazi wake kufanya hivyo kwa imani kuwa atafukuza roho
za kishetani na mikosi inayomsonga.
Mbwa huyo
alitafutwa na baba mzazi wa mrembo huyo na kufanyika sherehe kubwa ikiwa
na vitendo vyote vinavyofanywa na ya bibi harusi na bwana harusi kwa
taratibu zao za ndoa.
Kwa mujibu wa Yahoo News, msichana huyo hakuwa na furaha kabisa na alieleza wazi jinsi alivyochukizwa na kitendo hicho, “Siifurahii kabisa hii ndoa.”
“Tulilazimika
kutumia pesa nyingi kwa ajili ya hii ndoa. Hiyo ndiyo njia pekee
tunayoweza kufanya kuondoa mikosi aliyonayo na kufanya tendo jema kwa
ajili ya kijiji chetu.” Amekaririwa mama yake Munda.BOFYA KUONA PICHA ZA HARUSI HIYO>>
No comments:
Post a Comment