BINTI mmoja aliyeonekana kuzidisha kiburudisho, mwishoni mwa wiki iliyopita alitibua
onyesho na kugeuka kuwa burudani baada ya kupanda juu ya jukwaa la
Mlimani Park ‘Sikinde Ngoma ya Ukae’ na kuwakumbatia ovyo
wanamuziki.Binti akivamia jukwaa baada ya kupiga urabu wa kutosha. Tukio
hilo lilitokea wiki iliyopita katika ukumbi wa Railway Club ambako
paparazi wetu alimshuhudia
binti huyo aliyefahamika kwa jina moja la Fatma, akianza kubadilika
taratibu kadiri alivyokuwa akipata kiburudisho chake kilichokuwa katika
vipakti vya plastiki.
Akizidi
kusumbua jukwaa. Licha ya kuwakumbatia, pia msichana huyo alivuruga
shoo hiyo baada ya kukanyaga nyaya zinazounganisha vyombo vya muziki vya
bendi hiyo na kusababisha umeme kuzimika jukwaani, hivyo kusababisha onyesho kusimama kabla ya mafundi mitambo kurekebisha hitilafu.
No comments:
Post a Comment