Kijana
mmoja aliyefahamika kwa jina la Marck Costantine (24), mkazi wa mtaa wa
Kitangiri jijini Mwanza amenaswa ‘live’ gesti akiwa na mke wa kigogo
mmoja (jina kapuni), aitwaye Mwanaidi wakijiandaa kuvunja amri ya sita.
Baada
ya fumanizi kati ya Serengeti boy aliyefahamika kwa jina la Marck
Costantine na mke wa kogogo. Tukio hilo lilijiri Septemba 18, mwaka huu
kwenye gesti moja maarufu iliyoko mitaa ya Kitangiri baada ya kigogo
huyo kupewa ‘ubuyu’ kwamba anaibiwa mali yake ndipo akaandaa mtego na
kufanikiwa kumnasa kijana huyo alipokutwa kwenye chumba namba 4 cha
gesti hiyo akijiandaa kuserebuka. “Kigogo alipopewa mchoro huo na
wambea, siku ya tukio alimshtua Mwenyekiti wa Mtaa wa Kitangiri, Maginga
Patroba, wakatia timu katika gesti hiyo, wakawakuta wachepukaji hao
wakiwa kitandani huku Marck akiwa tayari ameshachojoa nguo, Mwanaidi
akiwa bado,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
Akisainishwa
kulipishwa faini. “Kigogo aliamuru wahudumu wagonge mlango ili wahusika
wasishtuke, walipofungua ndipo mwenyekiti sabamba na kigogo huyo
wakazama ndani.”
Mwanaidi alipoona flashi za kamera ya mapaparazi zikiwamulika,
alianza kuangua kilio mbele ya mumewe kumuomba awasamehe lakini kigogo
huyo alimtaka kijana huyo amlipe fidia ya shilingi milioni moja kama
adhabu ya kutembea na mke wake.
Kutokana na hali ya uchumi ya kijana huyo kutokuwa nzuri, hakuweza
kulipa kiasi hicho cha pesa badala yake aliomba kupewa muda wa kulipa
pesa hizo.
Barua ya makubaliano ya kulipwa pesa kwa kigogo huyo shilingi laki
tano. Chini ya uangalizi wa mwenyekiti, Marck aliandika barua ya
makubaliano jinsi ya kulipwa kwa kiasi hicho cha pesa kwa kigogo huyo na
iwe kama fundisho kwake kuachana na tabia za kutembea na wake za watu.
Kwa upande mwingine, mwenyekiti Patroba alikiri kumfahamu Marck na
kudai ni kijana wa mtaani kwake na kumuonya asirudie mchezo huo mchafu.
Mke huyo wa Kigogo aliyefahamika kwa jina moja la Mwanaidi akiwa analia akiomba msamaha kwa mumewe.
“Namfahamu huyu kijana nimeshangazwa na kitendo hiki anachokifanya
kwani ni vitendo ambavyo havikubaliki katika jamii hivyo kama kiongozi
wa mtaa huunitaendelea kutoa ushirikiano ili kuukomesha tabia kama hizi
za kuvunja miji ya watu,’’ alisema Patroba.