Panadol
wa Basajja amewekwa rumande kwa kusambaza picha chafuMsanii wa muziki wa
kizazi kipya nchini Uganda Kansiime Jemimah maarufu kama -Panadol wa
Basajja- amepelekwa rumande baada ya kukanusha mashtaka ya kusambaza
picha za uchi kinyume na sheria za nchi.'Panadol wa wanaume' ambalo ni
jina la kisanii la mwimbaji chipukizi wa Uganda-Kansiime Jemimah
amepelekwa rumande baada ya kukanusha mashtaka hayo.Msanii huyo wa kike
alikamatwa pamoja na mtengezaji wa muziki wake mwezi uliopita kwa kile
waziri wa maadili anasema ni kuhusiana na picha za uchi.
Panadol ametoa vibao kadhaa katika mahadhi ya kufoka lakini ule ambao umemletea shida unaitwa Ensolo Yange yaani mnyama wangu.
Katika
video ya wimbo huo kuna sehemu ambapo yeye mwimbaji akiwa kama mhusika
mkuu anaonekana akivaa chupi ya G-string huku makalio yake yakiwa nje.
Na pia kuonyesha mapaja yake na baadhi ya maneno ya muziki wake yakiwa
Kwa baadhi wanatafsiri maneno na picha hizo vingine na serikali kusem ani kinyume na sheria
Mwaka
jana sheria mpya dhidi ya picha chafu ilipitishwa ambapo ni marufuku
kuuza au kupatikana na picha za uchi. Adhabu ya mtu anaepatikana na
hatia ni faini ya shilingi za Uganda laki mbili sawa na dola nane au
kifungo cha miaka mine au vyote viwili.
Video
hiyo ya utatanishi ilitayarishwa na kijana Muchwa Mugisha maarufu kama
Didi ambae yeye alikiri kosa hilo 28 Oktoba na kuwekwa ndani na bada
kulipa faini, lakini Panadol akakanusha madai hayo na ndio leo ameletwa
mahakamani lakini pia kwa mara nyingine amekanusha madai hayo na hiyo
kurejeshwa rumande hadi Disemba 2 mwaka huu.
Sheria
hii ya picha za ngono mwanzo ilizusha mgogoro kwani ilipewa jina la
sketi fupi na baada ya watu kulalamika kipengee cha sketi fupi
kikatolewa.
No comments:
Post a Comment