Mtangazaji wa Kipindi wa Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida' akimlisha keki Shemeji yake, Feisal.
SIKU chache
baada ya kudai hawezi kuolewa kwa sasa, mtangazaji wa Kipindi cha
Mitikisiko ya Pwani kupitia Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’,
ameonesha matumaini mapya ya kuolewa baada ya kumwanika mchumba’ke mpya.Dalili
za matumaini hayo mapya zilionekana usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita
katika sherehe yake ya kuzaliwa (bethidei) iliyofanyaka nyumbani kwake,
Mwananyamala jijini Dar na kuhudhuriwa na mastaa kibao Bongo.
Khadija Shaibu ‘Dida' akiwa na mashemeji zake kutoka Arusha.
Miongoni
mwa wasanii waliohudhuria hafla hiyo ya kufuru ni pamoja na malkia wa
Mipasho Bongo, Khadija Kopa na waigizaji; Chuchu Hans, Jacob Steven
‘JB’, Rose Ndauka, Salma Salmin ‘Sandra’, Steven Mengere ‘Steve
Nyerere’, Jeniffer Kyaka ‘Odama’, Maimatha Jese na wengine kibao ambao
walimpa Dida kampani ya nguvu na kumtunza fedha na zawadi mbalimbali.
Shemeji, Feisal (mwenye kipaza sauti) akiwasilisha ujumbe alioagizwa na mume mtarajiwa kwa 'Dida'.
Kama
hiyo haitoshi, kwenye hafla hiyo, kulitawaliwa na vinywaji vya kila
aina huku kukiwa akichinja mbuzi watatu maalum kwa ajili ya sherehe hiyo
sambamba na kuku kibao wa kienyeji, nyama za kila aina, msosi wa nguvu
na pombe za kumwaga.
Miongoni mwa wageni waalikwa walikuwepo wasanii wa Filamu Bongo 'Chuchu Hans' na 'JB' .
Wakati
sherehe ikiendelea, Dida aliibua minong’ono ya aina yake baada ya
kutambulisha uwepo wa shemeji zake waliotoka Arusha ambao walimwakilisha
mchumba wake katika pati hiyo.
“Jamani
humu ndani kuna watu mbalimbali ambao wamefika kuniunga mkono, mkiwemo
wasanii wanahabari pamoja na watangazaji wenzangu, lakini kikubwa zaidi
napenda kutambua uwepo wa shemeji zangu waliofunga safari kutoka Arusha,
wamekuja kuniunga mkono, nimefurahi sana,” alisikika Dida.
'Dida' akilonga machache kwenye Shrehe hiyo ya bethidei yake.
Ulipofika
muda wa kutoa zawadi, mmoja wa mashemeji zake hao aliyejitambulisha kwa
jina la Feisal alishika kipaza sauti na kusema alitinga kwenye hafla
hiyo kumwakilisha ndugu yake (jina alilihifadhi) ambaye alimtuma
amwambie Dida kuwa amemzawadia gari lenye thamani ya Sh. milioni 26 za
madafu ambalo siku si nyingi litatua Dar.
“Hehee my new baby, huyo ndiye my new baby jamani na hawa ndiyo mashemeji zangu wa ukweli,” alipaza sauti Dida.
Ezden Jumanne wakati akiwa na 'Dida.'
Alipoulizwa na mwandishi wetu juu ya mipango yake na mchumba huyo mpya, Dida alifunguka:
“Huyo
ndiye mwanaume wangu wa sasa muda ukiwadia nitaanika kila kitu, bado
mapema mno kuzungumza mengi,” alisema Dida ambaye kama ataolewa na
mwanaume huyo itakuwa ndoa ya nne.
Dida
aliyemwagana na Ezden Jumanne miezi kadhaa iliyopita, kabla ya hapo
aliwahi kuolewa na wanaume wawili tofauti ambao alimwagana nao kwa
talaka.
No comments:
Post a Comment