WAKATI
bebi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiugulia maumivu ya
kuzomewa na mamia ya mashabiki wa muziki katika Tamasha la Fiesta jijini
Dar es Salaam mwishoni mwa wikiendi iliyopita, Wema Sepetu ‘Madam’
anaponda raha ya maisha nchini China, Amani lina full data.Bebi wa
mbongo Fleva ‘Diamond Platnumz’ , Wema Sepetu ‘Madam’. Chanzo makini
kilicho ‘kloz’ na muigizaji huyo nyota wa filamu nchini, kimesema Wema
alipaa na ndege ya Emirates wiki iliyopita, siku chache kabla ya Tamasha
la Fiesta, akiwa
ameandamana na wanaume wawili, ambao ni meneja wake, Martin Kadinda na Petit Man, wote wakiwa wamekaa daraja la kwanza la dege hilo. Chanzo hicho kilizidi kunyetisha kuwa gharama zote za safari hiyo zilibebwa na Madam mwenyewe na kwamba baada ya kufika katika jiji la Guangzhou nchini humo, Wema na wanaume hao wawili walichukua vyumba katika Hoteli ya Holiday Inn, inayotajwa kuwa moja ya hoteli ghali zaidi huko China.

“Yaani
Wema jamani ana mambo, inavyoonekana lile rhumba la wakati ule
ameshalisahau, amesahau kabisa kama alishafulia, sasa Mungu kamjaalia
kapata pesa anavyoitapanya ovyo mpaka roho inauma. Wewe fikiria mtu
amekwenda kuchukua vifaa vya biashara, unakwenda na hao wanaume wa kazi
gani kama siyo kupoteza fedha tu,” kilisema chanzo hicho.
Wema
Sepetu ‘Madam’ akipozi. Inadaiwa kwamba kilichompeleka Wema katika nchi
hiyo yenye watu wengi zaidi kuliko yoyote duniani, ni ununuzi wa
vipodozi, kwani ana mpango wa kufungua duka kubwa katika eneo ambalo
halijatajwa jijini Dar es Salaam.
Baada ya
kufika huko, chanzo kinasema kuwa watu hao watatu wamekuwa wakiishi
maisha ya starehe, wakila bata katika klabu mbalimbali za usiku, ambako
wanajichanganya na watanzania wengine kuponda raha.
“Kwa
matanuzi anayofanya kule, hata hiyo biashara aliyoifuata haina maana,
angekuwa mtu mwenye nia ya biashara kweli, angetafuta tu hoteli ya
kawaida ili kubana matumizi aweze kuja na mzigo mkubwa, sasa wewe
mwenyewe fikiria, hii wiki ya pili sasa, tena na wanaume wawili
wanakutegemea, hizo pesa si kuzitapanya tu jamani,” kilisema chanzo
hicho kikionyesha kutofurahishwa na maisha ya staa huyo.
No comments:
Post a Comment