Pichani ni
mti unaodaiwa kunyanyuka ghafla baada ya kuanguka miaka mitatu
iliyopitakatika kijiji cha Mfuto kata ya Ufuluma ,ambapo wilaya ya Uyuwi
mkoani Tabora.
Katika
hali ya kushangaza huku kila mtu akifikiria yake baaya ya juzi huko
mkoani Tabora, kutokea tukio la aina yake ambapo inaelezwa kuwa mti
aina ya Msufi uliokuwa umeanguka yapata miaka mitatu iliyopita
umesimama ghafla tena kwa sauti kubwa ya mrindimo na kuwafanya
wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo.
Tukio hilo limetokea Oktoba 17,mwaka huu,katika kijiji cha Mfuto kata ya Ufuluma katika wilaya ya Uyuwi mkoani Tabora.
Inaelezwa kuwa mti huo wenye kipenyo cha futi 2 uliinuka na kuwa kama zamani baada ya kutokea upepo mkali katika kijiji hicho.
Wananchi walikusanyika kila mmoja akitaka kuchukua angalau gome la
mti huo kwa ajili ya dawa ama kumbukumbu , na haya ndio maajabu ya
Tanzania. BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment