Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph akizungumza
machache kabla ya kumkaribisha Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji
Francis Mtungi kuzungumza na washiriki 31 wa mtandao wa redio jamii
Tanzania (COMNETA) unaotekeleza mradi wa demokrasia na amani (DEP)
kuelekea uchaguzi mkuu 2015 wanaohudhuria warsha ya siku nne
inayoendelea mjini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MSAJILI
wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi amezitaka Redio za Jamii
kutokubali kutumiwa na vyama vya siasa vinavyotumia unyonge wa
watanzania kiuchumi kujinufaisha kisiasa.
Alisema
kwa kufanya maamuzi ya kutotumiwa na vyama vya siasa kutasaidia
kuepusha migogoro inayochochewa na taarifa za kishabiki za vyamja vya
siasa.
Jaji
Mutungi alisema hayo wakati akichangia mada tatu zinazohusu Sheria ya
Gharama za Uchaguzi 2010, Sheria ya Vyama vya Siasa na Kanuni za Maadili
ya vyama vya Siasa zilizotolewa kwa viongozi na wamiliki wa redio jamii
nchini katika warsha inayoendelea mjini hapa.
Aliwataka
washiriki wa warsha hiyo ya siku nne inayohusu utekelezaji wa mradi wa
kuendeleza majadiliano kwa njia ya amani kwa lengo la kukuza demokrasia
nchini,kutambua kuwa baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakitumia unyonge wa
kielimu na uchumi wa watanzania kuwaahidi mambo yasiyotekelezeka jambo
ambalo amesema ni matumizi mabaya ya uhuru wa taasisi.
Msaajili
wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mtungi akizungumza na wadau
wanaohudhuria warsha ya siku nne ya kutekeleza mradi wa uchaguzi
unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi
mkuu ujao unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP)
inayoendelea mjini Dodoma. Kushoto ni Afisa Miradi ya Mawasiliano,
Habari na Tehama wa shirika la kimataifa la sayansi, elimu na utamaduni
(UNESCO) Bwana Al Amin Yusuph na Katikati ni Msajili msaidizi kutoka
ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bw. Ibrahim Sapi Mkwawa.
Alisema
vyombo vya habari vya jamii bado visafi na vina nafasi kubwa
kubadilisha mitazamo ya utamaduni wa siasa chafu iliyojengeka kuwa
maendeleo ni kupata uongozi wa siasa, tena kwa kauli za uwongo na
kujenga chuki.
“Maendeleo
ni kuchagua kiongozi ambaye ni mwadilifu, mwenye uchungu na taifa na
yuko tayari kuitunza amani tuliyoirithi baada ya kupata uhuru wa nchi.”
alisema Jaji Mutungi.
Mada hizo ziliwasilishwa na Wasaidizi wa Msajili wa Vyama vya Siasa
Ibrahim Sapi Mkwawa, Sisty Leonard Nyahoza na Ofisa Sheria Mwandamizi
Piencia Etanga kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama Vingi vya Siasa.
Msajili
wa Vyama Vingi amesema, kwa kuwa Redio Jamii ndiyo zinazowafikia
watanzania wenye maisha ya kawaida walio wengi vijijini na ndio
wanaofuatwa na wanasiasa wa namna hiyo ili wawaunge mkono nia zao bila
kujali maslahi ya wananchi.
Wadau
wa mradi wa uchaguzi wakifurahi jambo wakati Msajili wa Vyama vya Siasa
nchini Jaji Francis Mtungi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao.
Amezitaka
redio jamii kuunganisha nguvu ya pamoja na wadau wakuu wa mradi wa
uchaguzi kwa kuwaelimisha wananchi, kusema ukweli bila woga kitu chenye
manufaa kwa umma hasa kuhusu wanasiasa matajiri kutumia raslimali zao
katika kutafuta kura hali ambayo imeliingiza taifa katika wimbi la
rushwa na umaskini wa kupindukia.
Alisisitiza kuwa siasa ni ushindani na kushinda hivyo zisirubuniwe kirahisi kwa pesa ambazo sio msingi wa maendeleo.
“Pesa
sio msingi wa maendeleo, msikubali kurubuniwa wala kununuliwa na
wachache wanaotumia nguvu ya pesa. Silaha kubwa ni kuunganisha nguvu na
vyombo vya habari jamii tutafanikiwa kulijenga taifa.”
Wakati
huo huo ofisi ya Msajili wa Vyama Vingi imekuwa ikikabiliwa na matatizo
kutokana na udhaifu wa sheria ambao wanasiasa wamekuwa wakiutumia kwa
kutoa lugha chafu na za uchochezi ili waweze kuungwa mkono bila kujali
maslahi ya taifa.
Msajili
msaidizi kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bw. Ibrahim
Sapi Mkwawa, akiwasilisha mada ya Sheria ya gharama za uchaguzi ya
mwaka 2010 kwa wadau wanaotekeleza mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha
demokrasia na amani nchini (DEP) katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi
mkuu ujao, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP)
kwenye warsha ya siku nne inayoendelea mjini Dodoma. Kutoka kulia meza
kuu ni ........Sisty Leonard Nyahoza, Kamishna wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC), Jaji John Mkwawa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini
(RPP), Jaji Francis Mtungi wakisikiliza kwa umakini mada zilizokuwa
zikiwasilishwa kwenye warsha hiyo.
Mada
nyingine iliyotolewa katika mkutano huo wa siku nne uliofadhiliwa kwa
ushirikiano wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNDP na UNESCO
iliyofanyika katika Ukumbi wa Waziri Mkuu mjini Dodoma ni Jinsia na
Kuhusisha Makundi Maalum Katika Uchaguzi 2015 na Margareth Rugambwa
kutoka Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Kuwapatia Uwezo
Wanawake (UN Women).
Katika semina hiyo washiriki wameazimia kutumia redio jamii katika
kufanikisha mawasiliano baina ya wananchi na vyombo vinavyosimamia
masuala ya uchaguzi na siasa.
Msajili
Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty
Leonard Nyahoza, akiwasilisha mada ya Sheria ya Vyama vya Siasa kwa
wadau wa warsha ya mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na
Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu mwakani inayoendelea mjini
Dodoma kwenye ukumbi wa mikutano ofisi ya Waziri Mkuu.
Sehemu
ya washiriki wa warsha ya siku nne kwa wadau wa mradi wa uchaguzi 2015
unaolenga kuboresha demokrasia amani nchini (DEP)katika kipindi hiki
kuelekea uchaguzi mkuu ujao, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la
Maendeleo (UNDP) iliyoenda sambamba na mkutano wa tano wa Mtandao wa
vyombo vya habari vya Kijamii nchini (COMNETA).
Afisa
Sheria Mwandamizi Piencia Etanga kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa akiwasilisha mada ya Kanuni za Maadili ya vyama vya Siasa
zilizotolewa kwa viongozi na wamiliki wa redio jamii nchini katika
warsha inayoendelea mjini Dodoma.
Msajili msaidizi wa
Vyama vya Siasa nchini (RPP), Jaji Francis Mtungi (kulia) akiteta
jambo na mmoja wa wasaidizi wa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
nchini, Bw. Ibrahim Sapi Mkwawa (kushoto) kwenye washa ya siku nne ya
wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha demokrasia
na amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao inayofadhiliwa na
shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo (UNDP).
Mratibu
wa Mradi wa kuboresha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya Msajili
wa Vyama vya Siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano, akielezea utekelezaji
wa mradi huo unaoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini
chini ya ufadhili wa UNDP kwa wadau wa redio za jamii nchini.
Katibu
wa mtandao wa redio za jamii nchini (COMNETA), Bw. Abbas Mwakalinga
(kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Redio ya Jamii FADECO ya wilayani Karagwe, Bw.Joseph
Sekiku wakati wa warsha hiyo.
Meneja wa
Pambazuko FM Radio ya Ifakara, Bw. Joseph Kamata akihoji swala kwa wa
wasilishaji mada kwenye warsha hiyo inayoendelea mjini Dodoma.
Kutoka
kushoto ni Mshauri wa UNESCO na Mlezi wa mtandao wa redio jamii
(COMNETA), Balozi mstaafu Mh. Celestine Liundi, Mshauri na Mkufunzi
kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu pamoja na Afisa Habari na Mahusiano Tume
ya Uchaguzi Zanzibar, Bi. Salha Ali wakifuatilia kwa umakini mada
mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa.
Msajili
wa Vyama vya Siasa nchini (RPP), Jaji Francis Mtungi akibadilishana
mawazo na baadhi ya washiriki wa warsha ya siku nne inayoendelea mjini
Dodoma kwenye ukumbi wa mikutano ofisi ya Waziri Mkuu.
Mshauri
wa UNESCO na Mlezi wa COMNETA, Balozi mstaafu Mh. Celestine Liundi
(kulia) akibadilishana mawazo na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na
Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
Bw. Al Amin Yusuph wakati wakielekea kupiga picha ya pamoja na washiriki
wa warsha hiyo.
Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mtungi akifurahi jambo na rafiki yake wa siku nyingi Reportuer wa warsha ya wadau wanaotekeleza mradi wa uchaguzi inayoendelea mjini Dodoma Mchungaji Privatus Karugendo.
Msajili
wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mtungi, wakufunzi, wafanyakazi wa ofisi
ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakiwa kwenye picha ya pamoja na
washiriki.
No comments:
Post a Comment