Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (katikati) akiongoza
na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mtungi (kulia) baada
ya kuwasili ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi.
Kushoto ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la
Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi akimkaribisha ofisini kwake
Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues alipomtembelea na
kufanya naye mazungumzo. Kushoto ni Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.
Jaji Francis Mtungi na kushoto ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na
Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
Bw. Al Amin Yusuph na Nyuma kabisa ni Msajili Msaidizi kutoka Ofisi ya
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Leonard Nyahoza.
Mkurugenzi
Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues akisaini kitabu cha wageni
ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi alipomtembelea
leo na kufanya nae mazungumzo juu masuala mbalimbali ya maendeleo
likiwemo suala la elimu na changamoto zake katika mkoa wa Dodoma.
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mtungi (wa pili kulia)
akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi
(kushoto), Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues (wa
pili kushoto) pamoja na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa
Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al
Amin Yusuph, Msajili Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
nchini, Sisty Leonard Nyahoza walipomtembelea Mkuu huyo wa mkoa ofisini
kwake leo.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (wa pili kushoto)
akitoa maelezo ya kazi mbalimbali zinazofanywa na shirika lake ikiwemo
Mradi wa Micro Science Kits (MSKs) ulioendeshwa kwa miaka minne wa
kusaidia ufundishaji wa masomo ya sayansi kwa kufanikisha majaribio ya
maabara uliokuwa ukifadhiliwa na Shirika lake na kuendeshwa na Wizara ya
Elimu nchini katika shule 180 zilizopo katika wilaya 34 ambao
umemalizika hivi karibuni kwa mafanikio makubwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi katika picha ya pamoja na ugeni huo ofisini kwake mjini Dodoma leo.
Mkurugenzi
Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues akisisitiza jambo kwa Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi alipokuwa akigana nae mara baada
ya mazungumzo ofisini kwake mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment