Mtoto,
Samwel John akiwa na maumivu makali aliyoyapata baada ya kujeruhiwa kwa
kisu. Akizungumzia mkasa huo kwa masikitiko makubwa uliojiri hivi
karibuni maeneo hayo, baba mzazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa
jina moja la John alisema kuwa, siku ya tukio hilo alimuona hausigeli
huyo akiwa amemshika mkono mwanaye huku akiwa na majeraha kwenye jicho
na kichwani. Alisema alipomuuliza nini kimetokea, hausigeli huyo
alimjibu kuwa mtoto Samwel aligongwa na pikipiki.
Unyama!
Dada wa kazi (hausigeli), aliyetajwa kwa jina moja la Rachel, mkazi wa
Tabata-Shule jijini Dar, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuchukua
kisu jikoni kisha kumchomachoma nacho mtoto, Samwel John (4) anayeishi
nyumba ya jirani.
John
alisema kwamba, hausigeli huyo alimwambia kuwa mtoto alikuwa amegongwa
na pikipiki lakini mtoto alikataa huku akimnyooshea kidole yule dada wa
kazi.
No comments:
Post a Comment