Ni week ambayo imefatana na weekend iliyoacha kumbukumbu nzuri kwa watu mbalimbali waliohudhuria tamasha la Fiesta ambalo mwaka huu limechukua headlines za rekodi kubwa ya mahudhurio karibu kila sehemu lilikopita ambapo Dar es salaam idadi inagonga kwenye elfu 50.Ali Kiba alikua miongoni mwa wakali waliokubali mwaliko wa kutokea juu ya jukwaa hilo ambapo
Millard alipata nafasi ya kuongea nae Exclusive aelezee ni Wasanii gani waliomvutia baada ya kuonyesha kazi zao on stage.
Ameanza kwa kusema >>> ‘Nilichelewa kufika sikuweza kuwaona
kina Ommy Dimpoz, Vanessa na kina Young Killer lakini niliobahatika
kuwaona wote wamefanya kazi nzuri, nilimkuta Waje na Panto walifanya
vizuri japo ni nyimbo zao chache tunazijua’
Akiwataja wasanii wa Tanzania waliofanya vizuri Ali amesema
>>> ‘Mr Blue amenifurahisha sana, WEUSI wamefanya kazi nzuri….
kina Diamond wamefanya kazi nzuri pamoja na Linah’
No comments:
Post a Comment