Wanasiasa wanaendelea na shughuli za kampeni hii leo, ikiwa siku ya mwisho kabla ya kupiga kura ya maamuzi nchini Scotland.
Mnamo siku ya Alhamisi Scotland itapiga kura ya maoni kuamua iwapo itaendelea kuwa katika muungano na Uingereza au la.Pande zote mbili za kisiasa zimekuwa zikitoa maombi ya mwisho kwa wapiga kura.
Kiongozi wa kundi linalotaka Scotland kujitenga, Alex Salmond, amewaomba raia wajichukulie wajibu huu muhimu mikononi mwao.
Ushindani umekuwa mkali ingawa matokeo ya kura ya maoni yaliyotolewa na mashirika matatu ya kujitegemea yanaonyesha kuwa wale wanaotaka Scotland iendelee kuwa sehemu ya Uingereza wanaongoza na pinti nukta nne pekee.
No comments:
Post a Comment