Wadau mbalimbali wa mchezo wa basketball.
Wanahabari toka vyombo mbalimbali wakiwa katika mkutano.
Mchezo wa mpira wa kikapu (Basketball) unaonekana kufifia kwa muda,
kutokana na kutokuwa na ligi na michezo ya mara kwa mara, hivyo
Basketball Dar es Salaam (BD) inawaomba wadau, makampuni na wapenzi wa
mchezo huo, kujitokeza na kuwaunga mkono katika kukuza na kuendeleza
mchezo huo.
Aidha BD kwa kushirikiana na Azam Tv imeandaa usiku wa basketball,
utakaofanyika Septemba 12 mwaka huu kwenye uwanja wa ndani wa Taifa,
ambao utasindikizwa na michezo mbalimbali ikiwemo ya Slam Dunk, 3point
Shoot-Outs, Skills Challenge pamoja na Bongo Fleva.
No comments:
Post a Comment