welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Tuesday, 16 September 2014

''Nawaonea wivu Chelsea na Man U''


Nahodha wa timu ya soka ya Liverpool ya England Steven Gerrard amesema amekuwa anazionea wivu timu za Chelsea na Manchester United zikishindana katika mashindano ya kombe la klabu bingwa barani ulaya.
Majogoo hao wa Anflid watashuka dimbani siku ya Jumanne kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2009,kucheza na timu ya Ludogorets Razgrad ya nchini Bulgaria.
'Tumekuwa tukisia tamaa na kuhisi wivu kwa kiasi kikubwa kwamba hatutashiriki kinyang'anyiro hicho,'' alisema Gerrard ambaye alishinda taji la michuano hiyo mwaka 2005
Nimekuwa nikitamani sana kuwepo. Kila mtu anazubiri kwa hamu kusikia muziki,'' alisema Gerard.
Chelsea wameshinda kombe hilo huku Manchester United wakimaliza katika nafasi ya pili tangu Liverpool kushiriki michuano hiyo miaka tano iliyopita. ''

No comments: