October
18 ilikua ni siku maalum ya Wakazi wa Dar es salaam kula bata kwenye
msimu wa mafanikio ambao unapita mara moja kila mwaka kwenye mikoa
mbalimbali ya Tanzania.
Ilikua ni
good time ya ukweli sana Watanzania kumuona T.I kumuona Davido kumuona
Victoria Kimani na Waje pamoja na wasanii wengine wa kimataifa ambao nao
walihudhuria tamasha hili lililokuwa na watazamaji zaidi ya elfu
hamsini.
Miongoni
mwa wasanii waliopokelewa vizuri kwenye show hii ni pamoja na Mr Blue na
Micharazo,Ally Kiba,Weusi,Vanessa Mdee,Stamina pamoja na Diamond
Platnumz ambaye aliimba single 4 kwenye jukwaa hili.
Mashabiki
wengi wa Ally Kiba inasemekana walipanga kuzomea wakati Diamond
Platnumz anaperfoam pale jukwaani,kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm meneja
wa Diamond Platnumz aitwae Babu Tale kaongelea hali hii.
Hizi ni sentensi 4 alizozisema.
1.Sisi
tumechukulia sehemu ya mashindano,uzuri sisi tuliambiwa na uongozi wa
Clouds kabla ya Diamond hajapanda ilikua saa 3 kamili tukaitwa
tukaambiwa kuna watu wamejiandaa kumzomea Diamond.
2.Kama
uongozi tulikaa na msanii wetu na kumjenga kisaikolojia na kumwambia
kuna hivi vinatokea wao walitaka aanze Davido kisha afate Diamond
kupunguza watu watakaozomea tukasema hapana pangeni show yenu kama
ilivyokuwa ni sehemu ya mashabiki kufurahi.
3.Hatujaathirika
kwamba msanii wetu ameshuka tunapoona watu wanapiga kelele kwa ajili
yako au huna sifa ile unatakiwa uangalie umekosea wapi unaenda
wapi,hatuna makosa kwa mashabiki wetu.
4.Kikubwa
Diamond anafanya vizuri tunatakiwa kuhamisha macho yetu tumpigie kura
Diamond kwenye tuzo za Channel O Music Awards, kwa sababu mwisho wa
siku chema chajiuza kibaya chajitembeza
No comments:
Post a Comment