Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda akiwa mahakamani. (Picha na Maktaba).
Na Haruni Sanchawa
Kesi ya jinai inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
Tanzania, Sheikh Issa Ponda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro
imeahirishwa leo kwenye Mahakama Kuu Dar es Salaam hadi Septemba 22,
mwaka huu.
Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Ponda anakabiliwa na
mashtaka ya uchochezi kwenye maeneo mbalimbali mkoani humo, likiwamo la
kukaidi amri ya Mahakama ya Kisutu iliyomtaka awe mhubiri amani katika
jamii likiwa ni sharti la kifungo cha mwaka mmoja nje baada ya kumtia
hatiani katika kesi ya jinai mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment