Stori: Mwandishi Wetu
WAKATI hofu ya mauaji
ya wanawake ikiwa bado imetanda mkoani Arusha, mama mzazi wa mshiriki
wa shindano la Big Brother Africa, Feza Kessy ameponea chupuchupu baada
ya kuvamiwa na majambazi wawili kisha kuporwa fedha.
Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa, Feza Kessy.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka jijini humo, Feza
alisema mama yake aitwaye Rose Kessy alikutwa na masaibu hayo mchana wa
saa nane, Jumatano iliyopita akiwa hatua chache kutoka nyumbani kwake,
eneo la Boma ya Siara, Moshono.
“Watu wawili wakiwa na pikipiki walimsimamisha akiwa garini anarejea
nyumbani, wakamteremsha na kuanza kumsachi, wakachukua pochi yake ambayo
ilikuwa na shilingi laki tatu ndani. Wakati wanafanya tukio hilo watu
walikuwa wanatazama tu bila kufanya lolote.
“Watu wengine walipita na gari wakataka kusimama, lakini wakaonyeshwa bastola na kupewa ishara
ya kuendelea na safari. Yaani walikuwa wanafanya wakiwa hawana wasiwasi
utafikiri ni askari vile, hivi hapa ndiyo nimerudi kutoka polisi,”
alisema mshiriki huyo ambaye pia aliwahi kushiriki shindano la Miss
Tanzania miaka ya nyuma.
Alisema
wakati wa tukio hilo, mama huyo anayefanya kazi Mahakama ya Kimataifa
ya uhalifu wa kivita wa Rwanda (ICTR) alikuwa ameambatana na mtoto wa
msanii huyo wa Bongo Fleva, aitwaye Jayden mwenye umri wa miaka
mitano.Alisema baada ya majambazi hao kuondoka, Polisi walifika nyumbani
kwao kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment