Mtoto wa
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Miraji Kikwete usiku wa Nov 11
2014 ameeleza kuhusu ishu inayosambazwa kwamba anamiliki kampuni ya
Simba Trust iliyopo Australia akishirikiana na dada yake.Kufuatia tuhuma
hizo Miraji alipost maandishi akikanusha hiyo ishu akisisitiza kwa
eleweke hivi ningekuwa napokea milioni 100 kwa siku wallahi ningeshukuru
kwa mola ila siwezi kuchukua fedha kinyume na haki ninayo stahili’
‘Katika
jambo lililonishangaza ni hizi tuhuma za kuwa ninamiliki kampuni ya
Simba trust ya Australia mimi na dada yangu Salama, naona sasas
mmeishiwa hoja na kuanza kuzusha mambo, sijawahi kufika Australia na
sina kampuni ninayomiliki na dada yangu, lakushangaza kwanini PAP
wanilipe pesa bila sababu maalum’
‘Sina
pesa nyingi kiasi hicho, kidogo ninachokipata ni kwa jasho langu,
sijawahi na sitodiriki kupokea pesa ambazo si haki yangu kupata, acheni
kupandikiza chuki zisizo na ukweli wowote, atakaethibitisha basi na
aonyeshe hilo kwa vielelezo na ushahidi, chuki hazijengi, kweli
umeishiwa hoja na mambo ya msingi ya kujadili’
No comments:
Post a Comment