anayomiliki. “Tuliambiwa kuwa huyu bwana alikuwa akiishi maisha ya hali ya juu, sasa kutokana na tuhumza zake polisi wameanza kuchunguza kila alichonacho ili kujua uhalali wake,” kilisema chanzo. HALI tete, siku chache baada ya mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Muharani Mohammed Abdallah, maarufu kama Chonji kukamatwa na kutupwa gerezani kwa tuhuma za kukamatwa na dawa kulevya, sasa mali zake zimeanza kuchunguzwa.
Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa, kuna baadhi ya watoto wa vigogo
akiwemo mtoto wa meya mmoja wa zamani (jina tunalihifadhi), jijini Dar
es Salaam ambaye anadaiwa kuwa alikuwemo katika mkumbo wa kukamatwa
Chonji lakini alitoroka na sasa anasakwa na polisi.Kamanda wa Kikosi cha
Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini, SACP Godfrey Nzowa
alipotafutwa na gazeti hili ili afafanue madai hayo alisema uchunguzi wa
mali za wote wanaotuhumiwa kukamtwa na dawa za kulevya ni lazima
ufanyike. Chonji
akiwa chini ya ulinzi mkali na wenzake mahakamani. “Tunachunguza mali
zao wote waliokamatwa na tuhuma za dawa za kulevya na siyo kwa Chonji
peke yake, inapodhihirika kuwa ni za madawa huwa wanafilisiwa,” alisema
Kamanda Nzowa. Chonji na wenzake wanne walikamatwa usiku wa manane
Oktoba 21, mwaka huu nyumbani kwake Magomeni Mtaa wa Kondoa jijini Dar
na inadaiwa walikuwa na mzigo wa unga uliokuwa ukifungwa katika
vifurushi vidovidogo pia anadaiwa kukutwa na sare za jeshi (JWTZ) na
bastola.
No comments:
Post a Comment