Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya MrishoKikwete
ameondoka nchini usiku wa jana, Jumatatu, Septemba 15, 2014, kuanza
ziara ya wiki mbili katika Marekani ambapo atahutubia Mkutano wa 69 wa
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN General Assembly) New York.
Mbali na kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York,
Mjini New York, Rais Kikwete atashiriki katika mikutano mikubwa zaidi ya
10 ikiwa ni pamoja na kuhutubia Baraza Kuu wakati wa Majadiliano ya Jumla ( General Debate) yaliyopangwa kufanyika Septemba 24 hadi 27 na Septemba 29 hadi Oktoba Mosi, mwaka huu, 2014.

Rais Kikwete amepangwa kuwa kiongozi wa 12 duniani kuhutubia Baraza
hilo mchana wa Alhamisi ijayo, Septemba 25, 2014. Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utaanza Septemba 16 hadi Desemba 24, mwaka huu, Miongoni mwa mikutano mingine muhimu ambayo Rais Kikwete atashiriki ni pamoja na kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) Kuhusu Mazingira (CAHOSC) na Mkutano wa Wakuu wa Nchi Kuhusu Mazingira ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Mheshimiwa Ban Ki Moon.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
16 Septemba , 2014.
No comments:
Post a Comment