Stori: Musa Mateja, Tabora
OHOOO!
Mchumba wa staa wa Mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shishi Baby’, Naftari
Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukataliwa
‘ukweni’ kwao, Tabora.
Mchumba wa staa wa Mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shishi Baby’, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.
Tukio hilo lilijiri ndani ya Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini hapa
wakati wawili hao walipokuwa wakipafomu kwenye tamasha la Serengeti
Fiesta ndipo mashabiki waliposema hawamkubali Nuh na badala yake aolewe
na DJ Zirro.
Wakati shoo ya wawili hao ikiendelea, Shilole alikatisha muziki kwa
muda na kuwaambia mashabiki kupitia kipaza sauti wamwambie kama Nuh
Mziwanda ana vigezo vya kuwa mumewe ndipo wakasema hapana na
kumpendekeza DJ Zirro ambaye alikuwa akipiga muziki kwenye shoo hiyo.Staa wa Mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shishi Baby’, akiwa na mpenzi wake Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.
“Hatumtaki Nuh Mziwanda awe shemeji yetu, bora uolewe na DJ Zirro.
Sisi ndiyo tumeamua hivyo,” alisikika mmoja wa mashabiki waliokuwa
wakifuatilia burudani hiyo.
Kitendo hicho cha mashabiki kumkataa Nuh Mziwanda kilimfanya
bwa’mdogo huyo ambaye naye anaimba muziki wa Bongo Fleva kujikuta
akiropoka na kusema:“Kama mnadhani sina hela basi naomba nitoe mahari
hapahapa,” alisema Nuh huku akiwatupia mashabiki kiasi kidogo cha fedha.
Pamoja na kufanya hivyo, bado mashabiki waliendelea kumkataa Nuh
Mziwanda hadi aliposhuka jukwaani ambapo alionekana kukwazwa na jambo
hilo kwani tokea aliposhuka alikosa raha kabisa.
Paparazi wetu
alimfuata Nuh Mziwanda alipokuwa ameketi baada ya kushuka jukwaani na
kumuuliza amejisikiaje kukataliwa ukweni, akafunguka:Staa wa Mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shishi Baby’,
“Kusema kweli kuna muda nimejisikia vibaya ingawa hapohapo jukwaani
nilijifikiria na kugundua kuwa ni gemu tu hivyo nimejifariji kwa kuona
kama ni sehemu ya burudani tu,” alisema Nuh Mziwanda.
No comments:
Post a Comment