Msanii
Rose ndauka akizungumza na waandishi wa habari juu ya ushiriki wao
kwenye tamasha kubwa la filamu litakalofanyika jijini Tanga jumamosi ya
wiki hii na kuwashirikisha wasanii wote wa kundi la Bongo Muvie kuliani
shamsa ford na wasanii wengine.
====== ======= =======
TAMASHA
la wazi la filamu Tanzania “Grand Malt Film Festival 2014” sasa
litafanyika kuanzia Oktoba 4hadi 8 mwaka huu kwenye viwanja vya
Tangamano jijinia Tanga imeelezwa.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL), Fimbo Butallah, alisema kuwa maandalizi ya tamasha hili
yamekamilisha na uzinduzi rasmi utafanyika Jumamosi Oktoba 4 na mgeni
rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Halima Dendegu.
Butallah
alisema kuwa tamasha hilo ni la wazi na hakuna kiingilio kwa wadau wa
Sanaa hiyo ya filamu na uzinduzi utafanyika kuanzia saa tisa mchana.
Alisema
kuwa kabla ya uzinduzi wa tamasha hilo, wasanii mbalimbali nyota ambao
wanatarajia kushirikishi tamasha hilo watafanya kazi ya jamii kwa
kutembelea kituo cha watoto wenye matatizo ya ngozi.
Aliongeza
kuwa kupitia tamasha hili Grand Malt inasaidia kuinua na kutangaza kazi
za wasanii wa hapa nchini na kuwapa nafasi ya kuwakutanisha na wadau na
mashabiki wao.
Naye
Kaimu Mwenyekiti wa Bongo Movie, Single Mtambalike, aliishukuru Grand
Malt, kwa kufanikisha tamasha hili kwa mwaka wa tatu mfululizo.
Mtambalike
alisema kuwa Sanaa ya filamu inasaidia kuwapatia ajira watu mbalimbali
hapa nchini na kutaja katika maandalizi ya filamu moja, Zaidi ya wasanii
50 wanatumika kucheza filamu hiyo.
“Tunaashukuru
sana Grand Malt na Sophia Records kwa kufanikisha tamasha hili ambalo
linathibitisha wazi kuwa tasnia hii ni biashara kubwa”, alisema
Mtambalike.
Rose
Ndauka, ambaye naye ni msanii ya filamu aliwataka wadau wote kujitokeza
na kutaja moja ya vitu watakavyotoa kwa watoto watakaowatembelea ni
magodoro 60.
Awali tamasha hilo lilipangwa kufanyika mapema mwezi Agosti mwaka huu mkoani Mtwara.
No comments:
Post a Comment