welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Monday, 13 October 2014

DIAMOND AZUNGUMZIA TOFAUTI YAKE NA ALI KIBA


Diamond na Alikiba ndio wasanii wa bongo fleva wenye timu mbili kubwa za mashabiki waliogawanyika na kuwashindanisha kwa niaba yao, Team Diamond v/s Team Alikiba, ushindani ambao umevalishwa ‘mask’ za ‘beef’ ambayo Nasib Abdul amedai kuwa haipo.Platnumz ambaye alikuwa bado hajaamua kuzungumzia tofauti hizo ameamua kufunguka juu ya ushindani pamoja na ‘beef’ iliyokuwa inazungumzwa baina yake na muimbaji huyo wa ‘Mwana’. 
“Nimekua nikiskia muda mrefu vimezungumziwa sana, kwenye mitandao katika nini, sijui kwanini vinazungumziwa hivyo” aliiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm “Unajua kuna time ikifika inabidi uangalie na kuna vitu uvizoee tu sababu havikuanza leo hivi vitu sio tu kwa Ali, ukiwa unafanya vizuri ni msanii yeyote ambaye atakuwepo nae anafanya nyimbo au akatoa nyimbo yaani utakuja utashindanishwa nae tu, atakuja huyu na huyu na huyu, lakini wewe mwenyewe tu kuangalia heshima yako iko wapi kuangalia kazi zako unazifanyaje ubora wake”. “Tangia mwanzo yaani inavyoanza ishagatokeaga hivyo ilikua sijui kwa Belle 9, ilitoka kwa Belle 9 ikaja nafikiri sijui Sam Wa Ukweli ilikua, ikaja sijui kwa Bob Junior, ikaja pia kwa Ali, ikatoka kwa Ali tena ikaja ikaondoka ikaenda kwa Omary I mean Ommy Dimpoz, ikatoka tena ikaja kwa Richard Mavoko, so kila time inavyokuwa inaenda unafanya vizuri hivyo vitu vinakua vinatokea, so ni we mwenyewe kuangalia na watu wasiokuwa na upeo wanaweza wakahisi hawa watu wana tatizo kumbe si tatizo ni vitu ambavyo vitakuwepo tu kwasababu mashabiki wana tabia wakiona mtu anafanya hichi na we unafanya kitu mkiwa katika kazi inayofanana hivyo vitu vitatokea yaani watu watashindanisha, unaweza hata ukashindanishwa na mtu ambae hata hakufikii kiwango kabisa”.“Hata kwenye boxing ipo, ukiangalia hata kuna kipindi ilikuwa TMK na East Coast, ilikuwaga kwa Dully na T.I.D hivi ni vitu vya kikazi hata kwenye mpira ndio maana kuna Simba na Yanga, lakini haimaanishi Simba na Yanga ni maadui wakikutana Ngassa ntakupiga ngumi au flani ah ah..”

No comments: