Kapteni
Emmanuel Kukula (aliyenyoosha kidole) wa Jeshi la Wananchi Tanzania
akiwa na baadhi ya maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa pamoja na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa
Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu wakishauriana masuala ya Protokali
kabla ya kuanza kwa sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa
Mataifa tangu kuanzishwa kwake zilizofanyika leo jijini Dar es Salaam
kwenye viwanja vya Karimjee. (Picha na Zainul Mzige)
Na Mwandishi wetu
WASHIRIKA
wa maendeleo wametakiwa kutimiza ahadi yao ya kuwezeshwa kuanzishwa kwa
mfuko wa mabadiliko ya hali ya hewa (GCF) kwa kuchangia dola za
Marekani bilioni 100 kila mwaka hadi kufikia mwaka 2020.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi
Profesa Anna Tibaijuka wakati wa sherehe za Umoja wa Mataifa kufikisha
miaka 69 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Aidha
alisema ni muhimu pia watekeleze ahadi ya fedha, uhamishaji wa
teknolojia na uwezeshaji ili mataifa yanayoendelea yaweze kuhakikisha
kwamba yanabadili mifumo yao ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya
hewa.
Katika
sherehe hizo zilizofanywa kwa shamrashamra kubwa pamoja na gwaride,
Profesa Tibaijuka alisema juhudi hizo zinazoelekezwa na Umoja wa Mataifa
hazina budi kufuata kanuni za Rio ambapo kuna nia moja ya kukabili
mabadiliko ya hali ya hewa na wajibu tofauti.
Aidha
alisema pamoja na Tanzania kutekeleza wajibu wake inaamini kwamba
viongozi wa wadunia wakiwa mstari wa mbele katika mkutano ujao wa Lima
ambao unaandaa mkutano wa Paris mwakani watawezesha makubaliano bora
yanayotekelezeka.
Brigadia Jenerali Dominc Basil Mrope wa JWTZ (kushoto) akiwasili kwenye viwanja vya Karimjee na kuelekea jukwaa kuu.
Pamoja
na kuzungumzia uwajibikaji katika masuala ya kukabili mabadiliko ya
tabia nchi Waziri Tibaijuka alizungumzia mafanikio ya Tanzania katika
kutekeleza malengo ya milennia na kusema kwamba yale yaliyobaki
yataendelea kufanyiwa kazi ili kusukuma mbele zaidi maendeleo.
Alisema
serikali kwa sasa imelenga kuendeleza yale ambayo hayajakamilika kwa
kutengeneza mpango wa maendeleo unaoana na malengo ya milennia
yaliyobaki.
Awali
akimkaribisha Waziri, Mratibu mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa shirika la maendeleo la UNDP, Alvaro Rodriguez, alisema
yapo mambo ambayo bado yanalegalega katika utekelezaji wa malengo ya
milennia na Umoja wa Mataifa utaendelea kuisaidia Tanzania
kuyakamilisha.
Alisema
pamoja na Tanzania kupiga hatua kubwa katika masuala ya elimu ya msingi,
usawa wa jinsia, vifo vya watoto, uzuiaji wa maambukizi ya Ukimwi na
kufanikisha upatikanaji wa maji safi na salama bado kuna changamoto
kubwa katika kukabiliana na umaskini na vifo vya wanawake katika uzazi.
Balozi
wa Sweden nchini Tanzania Mh. Lennarth Hjelmaker akiwasili kwenye
viwanja vya Karimjee na kupokelewa na afisa kutoka Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kuelekea jukwaa kuu.
Rodriguez
amesema kwamba mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa sasa yanasaidia katika
kukabiliana na upungufu katika maeneo husika huku wakisubiri
majadiliano na serikali kuhusu mipango ya maendeleo baada ya kupita kwa
muda wa mwisho wa malengo ya milenia.
Aidha
amesema kwamba kwa sasa kuna program 10 zinazofanywa na mashirika ya
Umoja wa Mataifa kuimarisha demokrasia ya Tanzania na haki za binadamu,
makabiliano na Ukimwi vifo vya akina mama wakati wa uzazi na uimarishaji
wa ajira kwa vijana.
Akitaja
mafanikio ya mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Mratibu huyo
alisema kwamba asilimia 96 ya zahanati na vituo vya afya nchini Zanzibar
vimewezesha hudma za mama na mtoto na karibu kila kituo kina tabibu
mmoja anayeshughulikia masuala hayo.
Aidha mfumo wa haki za mtoto umeimarishwa na wakimbizi wapatao 60,000 Nyarugusu wamepatiwa haki za msingi kama maji na elimu.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushi (katikati)
akibadilishana mawazo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa
na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu
Gamaha(kushoto) kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa
Mataifa zilizofanyika leo kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar.
Mkuu
wa uendeshaji na ushauri wa Ofisi za Umoja wa Mataifa Tanazania
Bw.George Otoo akibadilishana mawazo na Mkuu wa Shirika la Kimataifa la
Uhamiaji (IOM) hapa nchini Bw. Damien Thuriaux kabla ya kuanza rasmi kwa
sherehe hizo.
Mgeni
rasmi Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna
Tibaijuka akiwasili kwenye viwanja vya Karimjee huku akiwa ameongozana
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Baadhi
ya wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wakiwa
wamejipanga tayari kumlaki mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya miaka 69 ya
Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake Profesa Tibaijuka. Kulia ni
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania,
Hoyce Temu akihakikisha Protokali zimezingatiwa.
Pichani
juu na chini ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez akimtambulisha mgeni rasmi Waziri wa Ardhi , Nyumba na
maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka kwa baadhi ya wakuu wa
mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini mara baada ya kuwasili kwenye
sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa
kwake.
Waziri
wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka
akipokea heshima ya wimbo wa taifa kabla ya kuanza rasmi kwa sherehe za
maadhimisho miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Waziri
wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka
akikagua gwaride maalum kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya
Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake zilizofanyika leo jijini Dar.
Waziri
wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka
akishuhudia bendera ya Umoja wa Mataifa ikipandishwa kama ishara ya
kuadhimisha miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Mshehereshaji
wa sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa Maulida
Hassan kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa akitoa mwongo wa hotuba mbalimbali kwa meza
kuu.
Mgeni
rasmi Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna
Tibaijuka akisoma risala kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya
Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake yaliyofanyika kwenye viwanja vya
Karimjee jijini Dar.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisoma
ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kwenye sherehe za
maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika kwenye viwanja
vya Karimjee jijini Dar.
Waziri
wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka
akipongeza Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez kwa hotuba nzuri.
Makamu
Mwenyekiti wa Asasi ya Umoja Mataifa (UNA), Bw. Benedict Kikove
akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa
Mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar.
Kwa picha zaidi ingia humu
No comments:
Post a Comment