Chanjo ya surua na rubella katika baadhi ya maeneo wilayani
Rufiji, Mkoa wa Pwani imekumbwa na changamoto mbalimbali, ikiwamo ya
baadhi ya wananchi kugoma kuwapeleka watoto wao katika vituo vya afya
kwa madai kuwa dawa hizo zinatolewa na ‘Freemason’ ili kuwafunga vizazi
Alisema mahudhurio ya wananchi katika vituo vya
chanjo vilivyopo maeneo hayo ni ya kusuasua, lakini kata nyingine
mwitiko wake ni mkubwa.
Dk Mollel aliwataka wananchi kupuuza maneno ya
mitaani ambayo hayana ushahidi wa kisayansi, badala yake wawapeleke
watoto kupata chanjo hiyo muhimu.
Alisema sambamba na chanjo za ugonjwa huo, pia
kutakuwa na utoaji wa matone ya vitamin A na dawa za kukinga magonjwa ya
minyoo, matende na ngiri maji.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin
Babu alisema amekerwa na wanaosambaza uvumi huo, huku akiwataka wananchi
kupuuzia taarifa hizo za mitaani.
“Hakuna Serikali yoyote duniani inayoweza kutoa dawa kwa ajili ya kuathiri watu wake,”alisema.
Alisema dawa hizo ni sahihi na salama zenye lengo la kulinda afya za watoto na hazina madhara kwa binadamu.
Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Donald Mbando
alikaririwa akisema kuwa, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inatarajia
kufikia watoto zaidi ya 21 milioni wenye umri kuanzia miezi tisa hadi
miaka 15.
Lengo la kampeni shirikishi ya ugonjwa wa surua na rubella ni kuhakikisha magonjwa yanayoepukika kwa chanjo yananatokomezwa.
Na Amini Yasini
No comments:
Post a Comment