Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zubeir Mtemvu.
LILE
sakata la Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zubeir Mtemvu kudaiwa
kudanganya limeingia ukurasa mwingine kufuatia ufukunyuku wa gazeti hili
kubaini kuwa, miaka 25 ndiyo sahihi kwake.
Kufuatia
ushindi alioupata siku ya shindano la kumsaka Miss Tanzania 2014
lililofanyika Oktoba 11, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Mlimani City,
kuliibuka madai kwamba mrembo huyo alidanganya umri.
Awali,
akiwa jukwaani kujitambulisha na kujibu maswali, mlimbwende huyo
alishika kipaza sauti na kusema:“My name is Sitti Mtemvu, ‘am eighteen
years old (jina langu ni Sitti Mtemvu, nina miaka kumi na nane).
Hapo
ndipo palipoanzia utata, wanaomjua Sitti walianika umri wake kwamba, ana
miaka 25 huku wakianika tarehe ya kuzaliwa kwake kwamba ni Mei 31,
1089. Miandao ikaanza kumponda kwamba alidanganya umri hivyo halimfai
tena!
Kufuatia hali ya hewa kuchafuka kwenye mitandao, redio na magazeti akishutumiwa Sitti, Oktoba 21, mwaka huu, mratibu wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga aliitisha mkutano na vyombo vya habari
No comments:
Post a Comment