Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasiliana na baadhi ya wananchi waliokuwa
wakimjulia hali kupitia simu yake ya mkononi kupitia ujumbe mfupi(sms)
leo Jumatatu.Rais Kikwete anayepata matibabu katika hospitali ya Johns
Hopkins jijini Baltimore Maryland nchini Marekani anaendelea vizuri na
anafanya mazoezi mara kwa mara na afya yake inaendelea kuimarika(picha
na Freddy Maro)
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana,
Jumatatu, Novemba 10, 2014, alianza kuwasiliana na mamia kwa mamia ya
wananchi mbali mbali nchini kujibu ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) wa
kumpa pole, kumtakia heri na nafuu ya haraka ambao amekuwa anatumiwa na
wananchi tokea mwishoni mwa wiki.
Tangu
alipofanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) Jumamosi iliyopita kwenye
Hospitali ya Johns Hopkins, Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani,
Rais Kikwete amepokea mamia kwa mamia ya SMS zikimpa pole na kumtakia
nafuu ya haraka.
Rais
Kikwete bado anaendelea kujibu SMS hizo na wananchi ambao wamemtumia SMS
Rais Kikwete waendelee kusubiri majibu ya Mhe. Rais kwa sababu
anakusudia kujibu SMS zote ambazo ametumiwa.
Aidha,
Rais Kikwete jana alizungumza kwa simu na uongozi wa juu wa Tanzania kwa
mara ya kwanza tokea afanyiwe upasuaji. Rais alizungumza na Makamu wa
Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar Mheshimiwa
Dkt. Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda.
Wakati
huo huo, madaktari wanaondelea kumtibu Rais Kikwete jana waliondoa
bandeji kwenye sehemu ambako alifanyiwa upasuaji wakieleza kuwa hali
yake inaendelea vizuri na anapata nafuu kwa kasi nzuri.
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
11 Novemba,2014
No comments:
Post a Comment