‘BEAUTIFUL Onyinye’, WEMA Isaack Sepetu ‘Madame’ ametoa ya moyoni
na kufichua kwamba maisha yake ya umaarufu anayoishi yanamtesa kwa
asilimia 40.
Pamoja na mateso hayo, staa huyo wa filamu alisema anafurahia
maisha yake kama mtu maarufu ikiwamo na kuandikwa na vyombo vya habari
mara kwa mara.
Unaweza Soma : Exclusive : Diamond kupewa PHD chuo kikuu cha mlimani, sasa ataanza kuitwa Doctor Nassib.
“Kuna wakati najutia kuwa maarufu kwa asilimia kama 40 hivi lakini nashukuru kwani kwa asilimia 60 nayafurahia maisha yangu.
“Ukiwa nyota kuna changamoto nyingi sana, kuna wakati mtu anaweza
kukuandika habari inayokufanya ushindwe hata kutoka nje na kubaki ndani
tu,”alisema.
Unaweza Soma : Je Ali Kiba kafata nyayo za Diamond kwa kutoa Tshirt hiziiii??? Zione hapa
Wema alisema kuna wakati huwa anatamani asingekuwa maarufu kwani
akifanya kitu kidogo hata kama ni cha kawaida lakini hupokelewa kama
habari kubwa na kuongelewa sana.
“Lakini katika maisha kama haya sina cha kufanya japo kuna mambo ambayo huniumiza na najitahidi sana kuvumilia,” alisema.
No comments:
Post a Comment