Pamoja na kujishaua mbele ya kamera za wanahabari na simu za
kuteleza (smart phones) kisha kutupia kwenye mitandao ya kijamii
wakizuga wapo pamoja, habari ya mjini inadai kwamba, sexy lady wa Bongo
Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ amemmwaga staa wa Ngoma ya
Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni rafiki mkubwa wa wapenzi
hao, ishu ya kumwagana ilikuwepo muda mrefu lakini kinachoendelea ni
kuwazuga mashabiki wao ili wasishuke kisanaa.
Chanzo hicho kilifunguka kwamba, siku chache zilizopita Wema au
Madam kama anavyopenda kuitwa, alimwambia Diamond kuwa anakwenda China
kuchukua mzigo bila kumwambia ni mzigo gani na kwamba huko aliambatana
na wanaume wanne, wawili wakiwa ni Martin Kadinda na Petit Man.
Ilidaiwa kwamba wanaume wengine wawili wapo kwenye mabano, jambo
ambalo Diamond au Dangote kama anavyopenda kujiita, hakuliafiki suala
hilo lakini Madam akasema liwalo na liwe yaani kama ‘mbwai iwe mbwai’
hivyo akampuuza na kwenda zake China!
Chanzo hicho kilidai kwamba, kuna wakati Madam alimuomba Dangote au
Chibu ampe fedha kwa ajili ya mtaji ambapo jamaa huyo alikubali lakini
siku zikawa zinayoyoma bila dalili hivyo Wema akaona wa nini kama mtu
mwenyewe hawezi kumsaidia?
Ilisemekana kwamba, baada ya kuona hali hiyo, Wema alijiongeza na
kuanza kukubaliana na makelele mengi kuwa jamaa huyo anamtumia
kibiashara huku yeye akilamba shoo na kupiga fedha ndefu ndani na nje ya
Bongo.
Chanzo hicho kiliendelea kumwaga ‘ubuyu’ kwamba, tabia ya Diamond
ya ubahili, nayo imechangia kwa Wema kukaa pembeni kwani jamaa huyo siyo
mkataji wa mkwanja kama ilivyokuwa kwa yule kigogo wa Wema, Clement.
“Wewe unamuonaje Wema? Yule mtoto bei mbaya bwana. Matunzo yake
si mchezo. Sasa Dangote na ubahili wake ndiyo hivyo atamsikia Madam
kwenye bomba,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilitiririka: “Unalikumbuka lile BMW (gari)
alilodaiwa Wema kapewa na Kadinda siku ya bethidei yake? Unajua Diamond
alikuwa Marekani, sasa aliporudi akataka kujua BMW imetoka wapi maana
yeye alitoa Murano, hapo ndipo moto ukawaka na wakawa hawaivani tena.”
Habari ziliendelea kupeperushwa kwamba siku ya bethidei ya Diamond
ambapo jamaa huyo alizawadiwa BMW X6 na uongozi wake wa Wasafi, Wema
alikwenda kwenye shughuli tu ili kuonekana kwenye kamera.
Ilisemekana kwamba, ndiyo maana kwenye shughuli hiyo Diamond ndiye
aliyekuwa akihaha kuhakikisha Wema hapati usumbufu tofauti na Wema
aliyekuwa anafuata tu maelekezo ‘kishingo upande’ kwani ndani yake
hakuna mapenzi tena.
Ilisemekana kwamba, baada ya tukio lile kulipita ukimya fulani huku
kila mmoja akiishi kwake tofauti na awali ambapo Diamond alikuwa
akijinasibu kuwa huwa analala nyumbani kwa baby (Wema), Mtaa wa Bwawani,
Kijitonyama jijini Dar.
Kwenye bethidei ya mwigizaji ambaye ni shosti wa Wema, Aunty
Ezekiel, Diamond ndiye alikuwa wa kwanza kuingia ukumbini kwenye Mgahawa
wa Rodizio uliopo Masaki jijini Dar, huku kukiwa na taarifa kwamba
Madam asingekuwepo kwa kuwa alikuwa safarini.
Wakati shughuli ikiendelea, Diamond alionekana mwenye furaha akiwa na timu yake lakini ghafla alipoibuka Wema upepo ukabadilika.
Wema alipoingia ukumbini akitokea safarini hata kabla ya kwenda
nyumbani, alimpita Diamond, akaenda kusalimiana na Aunty kisha akaanza
kuzunguka kwenye meza kusalimiana na mtu mmojammoja, cha ajabu alipofika
upande aliokuwa ameketi Diamond na timu yake, aliwaruka na kwenda moja
kwa moja kusalimiana na mwigizaji Jacqueline Wolper Massawe.
Ishu hiyo iliibua minong’ono kila kona ya ukumbi huo na
kuthibitisha zile tetesi kwamba hawapo kwenye uhusiano mzuri.Wakati Wema
akifanya yake na Aunty, Diamond alipishana naye kama hawajuani na
kukimbilia kwenye gari akiwa na timu yake tayari kwa kutimua.
Mwanahabari wetu alipotaka kujua kwa nini Diamond na ‘kruu’ yake
waliacha sherehe wakitaka kutimua, mmoja wa memba wa timu yake ya Wasafi
alisikika akisema ‘huyu demu siyo, hata ungekuwa wewe ingekuuma. Jambo
alilomtendea mshikaji siyo poa kabisa’.
Alipododoswa Wema juu ya kuzama kwake ukumbini na kumfanya Diamond
achomoke bila ya kusalimiana alishindwa kutoa majibu ya kina na kusema
hakujua nini kilimkimbiza ila yeye alikuwa pale kwa ajili bethidei ya
Aunt na si kingine.
Alipofuatwa Diamond kuzungumzia juu ya kutoka nduki baada ya Wema
kuingia ukumbini hapo, aliomba mwandishi wetu amwache kwa maana kwamba
ampotezee na kuzama kwenye ndinga lake na kuondoka kwa mbwembwe.
Hata kesho yake alipotafutwa kwenye simu yake ya mkononi ili aweze
kuzungumzia hilo hakuonesha ushirikiano kwani simu yake ya kiganjani
haikupokelewa muda wote alipopigiwa.
Penzi la Wema na Diamond limekuwa likigubikwa na sarakasi nyingi kila kukicha.
Wawili hao waliwahi kumwagana kipindi cha nyuma kisha kurudiana
Oktoba, mwaka jana. Kabla ya kurudiana, kijiti cha penzi la Diamond
kilikuwa kikishikiliwa na Mtangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’ huku cha
Wema kikiwa kwa yule kigogo wake, Clement.
No comments:
Post a Comment