Spika wa
Bunge Mhe Anne Semamba Makinda akipata maelezo toka kwa Katibu wa Bunge
la Oman,Ali Nasser Al Mahrouqi ya namna mfumo wa kisasa wa uendeshaji
Bunge ulivyo katika Bunge la Oman. Bunge hilo limeanza mfumo wa kutotoa
hotuba/nyaraka kwa makaratasi na sasa wanatoa kwa njia ya mtandao
(e-parliament).Wa pili kulia Mhe Sheikh Khalid Hilal All Maawali
akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Mhe Mussa
Zungu na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe.
Waziri wa
Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge Mheshimiwa William
Lukuvi akiongea na Spika wa Bunge la Oman Sheikh Khalid Al Maawali.Mhe
William Lukuvi ambae pia ni Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Bunge ni
miongoni mwa wabunge nane wanaoambatana na Mheshimiwa Spika katika ziara
rasmi ya kibunge nchini Oman.
Mhe Spika Sheikh Khalid Al Maawali akifafanua jambo kwa Mheshimiwa Spika Makinda kuhusu ukumbi wa Bunge la Majlis A'Shura.
Mheshimiwa Spika Makinda akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha Oman TV kuhusu ziara yake.
Mheshimiwa
Spika akimkabidhi zawadi ya picha ya mlango wa Zanzibar Spika wa Bunge
la juu la Oman Majlis Doula, Mheshimiwa Dr Yahya Al Mandhary.Mwingine
pichani ni Balozi wa Tanzania Oman Mheshimiwa Ally Saleh.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe akizungumza na Wabunge wenzake waliomo katika msafara.
Picha zote na Saidi Yakubu wa Ofisi ya Bunge.
No comments:
Post a Comment