KWELI ni
aibu nyingine! Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ Jumamosi
iliyopita alikumbwa na aibu nyingine kufuatia onesho lake kufanyika
ndivyo sivyo na hivyo kuzua tafrani miongoni mwa mashabiki wake mjini
hapa.
Aibu yenyewe iliyompata Diamond ilisababishwa na kuzimika kwa muziki
wake mara tatu katika onesho hilo na hivyo kuwafanya mashabiki kupiga
kelele hukuwengine wakidai pesa zao za viingilio.
Hali hiyo iliwafanya mafundi mitambo kurekebisha nyaya kwa zaidi ya
dakika 20 kila pale muziki ulipozimika hali iliyosababisha watu kuzidi
kupiga mayowe na kumtolea maneno ya shombo Diamond, wengine wakitishia
kumpopoa kwa mawe.
Muda mfupi baada ya mitambo hiyo kurekebishwa, mashabiki walianza
kuserebuka tena lakini baada ya dakika 45 muziki ulizima tena na
kusababisha mayowe mengine ya mashabiki wakiendelea kusema wameliwa pesa
zao.
Katika zomeazomea ya safari hii, mashabiki walikwenda mbele zaidi
wakimtaka Wema apande jukwaani kusalimia wakati mitambo ikirekebishwa
wakiamini Diamond alikwenda na bebi wake huyo kwenye onesho hilo.
Hata hivyo, mafundi mitambo waliingia tena kibaruani na kurekebisha mambo baada ya dakika 23 muziki ukaendelea.
MAIKI NAZO ZAKOROMA
Diamond alianza kufanya tena makamuzi ndipo maiki nazo zikaanza
kukoroma ambapo alianza kuwaomba wasaidizi wake wambabidilishie lakini
kila waliyompa ilikuwa ikikoroma na kuwafanya mashabiki wazidi kupandwa
na hasira.
“Haiwezekani bwana, huu ni ubabaishaji wa hali ya juu, mwandaaji gani
unaandaa shoo, unawachaji mashabiki kiingilio kikubwa halafu unashindwa
hata kuweka betri mpya kwenye maiki?
DIAMOND ABANWA NA RISASI JUMATANO
Kufuatia hali hiyo, baada ya shoo, Risasi Jumatano lilimfuata Diamond
na kumuuliza kulikoni muziki wake kuwa mwepesi pia kukatikakatika kila
mara hukumaiki nazo zikikoroma.
“Braza huu muziki siyo kabisa, huu ni muziki wa kupiga kwenye
vigodoro lakini siyo wa kufanyia shoo zangu hasa kama hii ambayo watu
wameingia kwa bei mbaya, ni kuwaibia watu.
“Mimi ni mtoto wa Kiislam ni lazima niongee ukweli, niliposikia
sehemu yenyewe ninayokuja kufanyia shoo inaitwa Matei Lounge nikajua ni
sehemu bab’ kubwa lakini kumbe ni ubabaishaji mtupu,” alilalama Diamond.
Katika intavyuu fupi, Diamond, alisema anadhani kama anahujumiwa
kwani haiwezekani muandaaji ashindwe kuweka vitu muhimu kwenye shoo.
alidai wanafanya hivyo wakijua inapotokea tatizo kama hilo anayejulikana
ni Diamond.
UJERUMANI, UINGEREZA
Ilianza nchini Ujerumani ambapo staa huyo alinusurika kudundwa
kufuatia vurugu zilizoibuka ukumbini alfajiri ya Jumapili ya Agosti 31,
mwaka huu baada ya kucheleweshwa kupanda stejini kwenye Ukumbi wa
Sindelfingen uliopo Mji wa Stuttgart.
KASORO YA DAIMOND NI MAMBO YA ‘USWAHILI’
Uchunguzi wa gazeti hili umegundua kuwa, Diamond licha ya kuwa msanii
mkubwa kwa sasa lakini bado anaendesha mambo yake ‘kiswahili’ sana.
Kama mambo hayo hayatakuwepo, msanii anaweza kugoma kufanya shoo.
Lakini mambo yote hayo hutakiwa kuwepo kwenye mkataba wa
makubaliano.Meneja wa Diamond, Babu Tale alipopigiwa simu juzi ili
kuulizwa kwa nini hakuwepo Dodoma kuhakikisha uwezo wa vyombo vya muziki
na maandalizi mengine, hakupatikana hewani!
No comments:
Post a Comment