Alilia sana kwa muda mrefu kwani alijua jinsi familia yake livyokuwa
ikimtegemea kutokana na mshahara wake. Baada ya kulia kwa muda
akakumbuka maneno ya kwenye maandiko matakatifu yasemayo,
" Binadamu hupanga mipango yake, lakini kauli ya mwisho ni yake Mwenyezi-Mungu. Matendo ya mtu huonekana kwake kuwa sawa,
lakini Mwenyezi-Mungu
hupima nia ya mtu. Mwekee Mwenyezi-Mungu kazi yako, nayo mipango yako
itafanikiwa. Mwenyezi-Mungu ameumba kila kitu kwa kusudi lake"
baada ya kukumbuka maneno hayo akajisemesha taratibu, " Mungu akiufunga
mlango mmoja, hufungua milango mingine mingi ya riziki kwa watu wake"
Kisha akanyanyuka na kuendele na kazi za nyumbani.
Siku moja akiwa anapita nyumba kwa nyumba, ofisi kwa ofisi akitafuta
kazi akakutana na kijana mmoja ambaye akamwambia, " Dada unaweza
kunisaidia kitu tafadhali ofisnini kwangu? Mhasibu wangu hajaja ofisni
kwa kuwa ameacha kazi bila kunipa taarifa na kwenda sehemu nyingine na
pia sina wakunisaidi.
Binti akasema, " Lakini kaka mimi mfanyakazi wa ndani sijui lolote
kuhusu masuala ya ofisini" Usijali nitakuelekeza kila kitu na kukupeleka
shuleni pia mpaka uelewe.
Binti akaanza kutokwa na machozi ya furaha huku akimwambia Mungu wake
asante kwa kuwa umenijibu sala zangu kwa kunizifanya ndoto zangu kuwa
kamilifu.
Funzo la leo
Mungu anaweza kukuinua kutoka sifuri mpaka kuwa mwenye kuheshimika na kukubalika kama utamtegemea yeye.
Comment AMEN kama waamini katika uwepo wa Mungu katika mafanikio yetu.
No comments:
Post a Comment