Mwanamke
wa Kikurudi na mwanae akiwa na bunduki aina ya AK-47 Tayari kuwakabili
wapigaji wa Dola ya kiislam wasiuteke mji wao kobane
Jengo
la gorofa likionekana kileleni bendera ya kundi la Isis ikipepea,katika
mji wa kobane,tukio hili limefanya kobane nzima kutaharuki.
Moshi mkubwa angani hii ni baada ya mashambulizi ya anga yakilenga sehemu ambazo inasemekana wapigaji wa Isis wamejificha.
Waturuki
wakijipiga picha mpakani kama kumbukumbu ,nyuma yao unaonekana moshi
ukipaa angani baada ya ndege za kivita za marekani kufanya mashambulizi
ya Anga.
Wana_nchi
wakituruki wanaoishi mpakani na Syiria,wamekuwa wajijitokeza kwa wingi
kushuhudia mapigano yanavyoendelea hasa jinsi jamii ja wakurudi
walivyojitokeza wote bila kujari jinsia umri nakubeba siraha kuulinda
mji wao usitekwe na Isis.
Wa_Turuki wakiangalia kwa mbali mapgano na hasa ndege za marekani zinavyofanya mashambulizi ya anga.
Mturuki akipiga picha kwa mbaali
Mpiganaji
wa Dola ya Ki_islaam akiwa na siraha yake mkononi,alikuwa akiongea
kwamba mafaniko yao yanatokana na uwezo waliopewa na Alah,na kwamba
hakuna wakuwazuia kuuteka mji wa kobane muda si_mrefu,na kuwateketeza
makafiri wote.
Wapiganaji wa ISIS wakiwa juu ya miinuko katika harakati zao za kuuteka mji wa kobane
Waturuki wakiangalia kwa mbaali mapigano kati ya kabira la wakurudi dhidi ya Isisasubuhi ya leo.
Habari kwa hisani ya mtandao wa Daiyl mail.
SYRIA-Licha
ya mashambulizi makubwa yanayofanywa na jeshi la anga la Marekani na
washirika wake dhidi ya wapiganaji wa Dola ya ki-islaam isis,rakini
wapiganaji hao wameweza kusonga mbele nakuukabili mji
uliopo mpakani,wako juu ya viunga na milima wakiuangalia kobane kwa
chini,
Kobane
ni Syria mji unaopakana na Uturuki ambao wakazi wake ni jamii ya
Kikurudi ,kabila linalojiona limebaguliwa huko katika nchi ya Uturuki na
mala nyingi wamekuwa wakitaka kutambuliwa kama Taifa huru bila
mafanikio,ni kabila lililopo katika nchi za Uturuki, Iraqi na Syiria.
Mapigano
ya leo asubuhi kati ya wanajeshi wa kikurudi wakisaidiwa na Marekani
zidi ya Isis imeleta taharuki kubwa kwa jamii nzima inayoishi katika huo
mji wa kobane,na wanaonakuna hatari mji wao wakati wowote kutekwa,na
kuangukia mikononi mwa isis ,hii inatokana na kusonga mbele katika
uwanja wa mapambano, kwa wapiganaji hao na wamefanikiwa kuteka milima
na viunga vinavyoikabili kobane,na wapiganaji hao wameapa kuuteka huo
mji na kuharibu na kuwaangamiza makafiri wote katika mji huo wa Syria
unaopakana na nchi ya uturuki,hali hiyo imewafanya wakurudi wote bila
kujali mtoto au mwanamke wameungana nakushika sira za aina mbalimbali za
kisasazikiwemo AK_47 kuulinda mji wao usiangukie mikononi mwa magaidi
isis,nae msemaji wa wapiganaji wawakurudi ,ameonya jamii ya kimataifa
kwamba iwapo isis itafanikiwa kuuteka mji wa kobane basi yanaweza
kutokea mauaji ya kimbari,na kwamba inatakiwa mikakati kuweza kuwazuia
isis wasiuteke huo mjiitakuwa vigumu kwa wapigaji wa _kikurudi kuwazuia
na kuwalinda wananchi wake iwapo Isis itafanikiwa yatatokea maafa
makubwa,
Nae
shuhuda aliyepo katika uwanja wa mapambano amesema kundi la isis baada
ya kuona linapata upinzani kutoka mashambulizi ya anga,limebuni mbinu ya
kutokwenda katika makundi makubwa kitu kinachofanya kuonekna na majeshi
ya Marekani nakushambuliwa kwa urahisi wamejiunda katika makundi
madogo madogo kitu kinachofanya Marekani kutokujua hasa wapi walipo,pia
isis wapiganaji wake wamekuwa wanaenda sambamba na vifaru vyao katika
harakati zao za kusonga mbele,
Wakati
yote hayo yakitokea uturuki imesogeza majeshi yake mpakani bila kutoa
msaada wowote ule,na wananchi wake wamejitokeza kwa wingi mipakani huku
ikiangalia tu , jinsi wapiganaji wa kikurudi wake kwa wa ume watoto
wazee walivyojiunga pamoja kuulinda mji wao kobane usitekwe ,imekuwa ni
sinema ya bure kuangalia kinachotokea alisikika mturuki mmoja aliyekuwa
na wenzake wakipiga picha upande wa pili ,huku ndege za Uingereza na
Marekani zikiendelea kufanya mashambulizi ya anga sehemu ambazo wanahisi
wapo wapinaji wa Isis.
Waziri
mkuu wa Uturuki amesema na kuonya kwamba mashambulizi ya anga
yanayofanywa na ndege za marekani ,hazijasaidia chochote kile na msaada
wake ni mdogo na nikama vile umechelewa wapiganaji wa kikurudi
wanaosaidiwa na marekani ni kama vile wamezidiwa nguvu na wapiganaj,i wa
dola ya kiislaam alisema waziri mkuu wa uturuki,yanahitajika majeshi ya
ardhini yaingilie kati upesi iwezekanavyo.
Bendera
za isis zimekuwa zikionekana zikipepea katka majengo marefu ya kobane
na viunga vyake kuashiria kwamba wakati wowote mji utakuwa chini ya
wapiganaji hao,Nao wapiganaji wa dola ya kiislamu katika mkanda wao
waliourusha hivi punde wamesikika wakisema na kujigamba kwamba mafanikio
yao waliyoyapata yanatokana na Alah kuwa upande wao ,pamoja
nakushambuliwa kutoka angani na majeshi ya Marekani na washirika wao
rakini Mungu wao Alah ananguvu kuliko Marekani na wameahidi kuuteka
kobane na kuwaangamiza makafiri wote alisema msemaji wao aliyekuwa
amebeba silaha.
No comments:
Post a Comment