“Filamu ya Kigoda ni filamu ya aina yake katika filamu ambazo
nimewahi kuzifanya,” alisema. “Filamu inahusu drama and music,
imeshagharimu pesa nyingi sana. Ndani utaona watu wakicheza muziki na
maisha ya wasanii. Kwahiyo itakuwa tayari hivi karibuni na tutatangaza
ikiwa tayar kwenda sokon.”
Katika hatua nyingine, Uwoya amekanusha uvumi kuwa ana uhusiano na
msanii wa Soundtrack, Msami ambaye anadai ameshiriki kwenye filamu hiyo.
“Msami sijawai kuwa na mahusiano naye, alikuwa kama msanii mwenzangu.
Hata ule ukaribu wake na mimi ambao ulizua tetesi za kuwa na mahusiano
naye ni kutokana na hii filamu. Kwa hiyo watu wajue ilikuwa ni kazi tu.”
No comments:
Post a Comment