Ni
shida! Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, chini ya
Kamanda Mohammed Mpinga, limekuwa mstari wa mbele katika kusimamia
maadili ya askari wake na kuwa mfano wa kuigwa lakini kuna baadhi
wanalichafua, kamchezo kamili kapo hapa.
Polisi wa usalama barabarani wakidendeka.
Habari kamili ikufikie kwamba nyuma ya picha ya askari wawili,
mwanamke na mwanaume wa usalama barabarani (matrafiki) wanaodaiwa kuacha
kazi ya kuongoza magari na kwenda kufanya uchafu kichakani kuna utata
mkubwa.
TUJIUNGE NA VYANZO
Baada ya picha hiyo kusambaa kwa kasi ya moto wa kifuu kwenye
mitandao mbalimbali ya kijamii usiku wa kuamkia Jumatano wiki hii na
kugeuka habari ya mjini, watu walikuwa na maoni tofauti huku baadhi
wakipiga simu kwenye chumba chetu cha habari wakitaka kujua ukweli juu
ya uwepo wa tukio hilo.
SIMU YA KWANZA
Simu ya kwanza iliyopigwa ilidai kwamba matrafiki hao ni maarufu
katika Barabara ya Bagamoyo ambapo mara nyingi huongoza magari maeneo ya
Tegeta jijini Dar.
Kamanda Mohammed Mpinga. “Huyo mwanaume ni jamaa mmoja mpole sana anajulikana Tegeta na ana gari aina ya Baloon (Toyota).
“Huyo mwanamke, kwanza ni mke wa mtu lakini yupo bomba (mzuri)
kinoma. Hata madereva daladala wanamjua maana amejaliwa, akitembea
lazima atingishe,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:
“Hapo ni maeneo ya Tegeta kwa sababu ukiangalia vizuri kwenye picha hiyo utaona nguzo ya umeme mkubwa wa Zanzibar.”
WHATSAPP
Wakati tukio likiwa ‘hot’, picha hiyo ilitumwa kwenye chumba chetu
cha habari kwa WhatsApp huku ikiwa na maelezo kwamba tukio hilo lilijiri
hivi karibuni mkoani Dodoma bila kufafanua maeneo gani kwa kuwa Dodoma
ni kubwa.
NI KANDA YA ZIWA?
Chanzo kingine kilichozungumza na gazeti hili kilidai kwamba tukio hilo siyo la Dar wala Dodoma ni maeneo ya Kanda ya Ziwa.
“Hilo tukio ni la Kanda ya Ziwa. Itakuwa ni kwenye moja ya Mikoa ya
Kanda ya Ziwa (kati ya Mwanza, Mara, Kagera, Shinyanga, Simiyu na
Geita),” kilidai chanzo hicho. (Ilishathibitishwa kuwa ni Kagera)
IMETENGENEZWA?
Baadhi ya wadau wa jeshi hilo walidai kwamba kuna uwezekano picha
hiyo ni ya kutengeneza (photo shop) kwa kuwa haikujulikana aliyeipiga na
kwamba iliwezekanaje kuwapiga ili hali wakijua ni kinyume na maadili.
“Unajua kinachonifanya nihisi kama imetengenezwa ni namna
walivyojiachia. Kwa vyovyote kuna kitu cha ziada kimefanyika kwenye hiyo
picha,” alisema mmoja wa wachangiaji mtandaoni.
MTAALAM: HAIJATENGENEZWA
Ili kuondoa utata huo wa kutengenezwa au kutokutengenezwa, gazeti
hili lilimwonesha picha hiyo, mtaalam wetu wa kompyuta (IT), Nicolaus
Trac ambaye alithibitisha kuwa siyo ya kutengenezwa.
“Ni vigumu kuwa ni ya kutengenezwa kwa sababu kuu tatu.
“Moja, mandhari ni moja, ingekuwa ya kutengeneza kila mmoja angeonekana tofauti lakini mazingira yanaonesha imepigwa eneo moja.
“Pili, angalia mikono yao ilivyovaana au kuingiliana. Sidhani kama
kuna mtaalam angeweza kuweka mikunjo hiyo ya mikono na vidole bila
kukosea sehemu.
“Tatu, angalia huyo mwanamke alivyomkalia mwanaume, inaonesha kabisa
kumkalia kwake kumesababisha mkunjo katika suruali kwenye paja la mguu
wa kulia,” alifafanua Nicolaus.
PETE YAIBUA MAMBO
Mbali na kukemea tabia hiyo na ukosefu wa maadili hasa kwa mtumishi
wa serikali, wapo baadhi ya watu mitandaoni walikuwa wakimshambulia
trafiki mwanamke kwani picha ilimuonesha akiwa na pete ya ndoa
kidoleni.
“Mimi sijui kama huyo trafiki ni mumewe lakini namuona ana pete ya
ndoa maana yake kuna harufu ya mchepuko. “Lakini hata kama ni mumewe,
kwa nini wafanye mambo ya chumbani hadharani tena na sare za kazi? Kama
walikuwa wamezidiwa sana si wangeenda nyumbani?” Alihoji mwanamke mmoja
aliyetumiwa picha hiyo kwenye WhatsApp.
KAMANDA MPINGA ANASEMAJE?
Gazeti hili lilimfowadia Kamanda Mpinga picha hiyo kwa njia ya
WhatsApp ambapo alikiri kuwa nayo na kwamba wanaifanyia kazi kabla ya
kuchukua hatua kali kwa wahusika.
Katika mahojiano ya Kamanda Mpinga hivi karibuni, kamanda huyo
alisisitiza kwamba kikosi chake kinaongoza kwa maadili na kwamba
inapotokea tukio kama hilo hutolewa adhabu kali.
No comments:
Post a Comment