MMH!
Katika hali ya kushangaza na kuonyesha kwamba ana hamu ya ndoa, msanii
wa filamu na muziki, Isabela Mpanda hivi karibuni alinaswa akitafuta
gauni la harusi wakati hata vikao havijaanza.Msanii wa filamu na muziki,
Isabela Mpanda. Kikizungumza chanzo makini kilisema mwanadada huyo
alikuwa maeneo ya Makumbusho jijini Dar akipita kwenye maduka mbalimbali
akitafuta gauni la harusi wakati hata maandalizi ya harusi yake na
Luteni Karama hayajaanza.Baada ya kuzinyaka habari hizo paparazi wetu
alimtafuta Isabela ambapo alikiri kusaka gauni hilo na kudai anajiandaa
kwa ndoa mwishoni mwa mwaka huu.
Luteni Karama akipozi. “Nina hamu sana ya kuingia kwenye ndoa ndiyo
maana naanza mapema, Mungu akijalia vikao vitaanza mwezi wa kumi, mwaka
huu,” alisema Isabela.
No comments:
Post a Comment