Mkazi wa Buguruni, Rukia Nassor amekimbilia Kituo cha Polisi Buguruni jijini Dar kutoa taarifa ya bintiye Saida Said (18) (pichani)kutoroshwa nyumbani kwake siku chache kabla ya ndoa.
Alipofika kituoni hapo, mwanamke huyo alimtaja mtu mmoja kwa jina moja la Shaban kwamba ndiye aliyefanya kitendo hicho.Akizungumza
na chanzo cha habari hizi, mmoja wa ndugu ambaye hakupenda jina
lakeliandikwe mtandaoni alisema mama huyo amekuwa akihaha kwa binti yake
kotoroshwa na mwanaume huyo tangu Septemba 25, mwaka huu ambapo kila
akimpigia simu hapatikana hewani
Jeshi
la polisi bado liko ndani ya msako mkali ili kuhakikisha binti huyo
anapatikana na hatua za kisheria zinachukuliwa kwa mwanaume huyo..
alisema ndugu huyo.
Ndugu
huyo alisema Saida alitarajiwa kufanyiwa ‘kitchen part’ Oktoba 31,
mwaka huu na kufuatia na ndoa Novemba 6 huku ikidaiwa kuwa, upande wa
bwana harusi michango inaendelea kama kawaida.
Jalada la uchunguzi kuhusu kutoroshwa kwa bi harusi huyo linasomeka Kumbukumbu; BUR/RB/10170/2014 KUTOROSHA.
No comments:
Post a Comment